Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mvua zaleta balaa Dar, Pwani
Habari Mchanganyiko

Mvua zaleta balaa Dar, Pwani

Daraja la Kiluvya
Spread the love

MVUA zinazoendelea kunyesha kuanzia jana mchana zimeanza kuleta madhara baada ya daraja la Kiluvya linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kukatika.

Kutokana na daraja hilo kukatika hudumza za usafiri  wa magari ya abiria, mizigo na binafsi umesitishwa na wananchi wameombwa kutumia barabara ya Bagamoyo.

Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ya Kaskazini, Kati, Kanda ya Ziwa,  Nyanda za juu Magharibu.

Daraja la Kiluvya

Aidha, mvua hizo zimesababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yamejaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.

Adha daraja lingine eneo la Mbezi beach jijini Dar es Salaam ‘maarufu la Jeshi’  kutokea Kawe limejaa maji na inadaiwa magari kadhaa yamezama na njia imefungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!