February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri wa Nishati ‘amtoa kafara’ mtumishi Tanesco

Waziri wa Nishati na Madini, Merdad Karemani

Spread the love

WAZIRI wa Nishati na Madini, Merdad Karemani amemtoa  ‘kafara’ meneja uendeshaji wa mtambo wa kufua umeme wa Kidatu mkoani Morogoro kufuatia nchi kuingia gizani mara kwa mara kwa kukosa umeme kuanzia jana, anaandika Hamis Mguta.

Amefanya maamuzi ya kumtimua mtumishi kazi mtumishi huyo wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), leo alipofanya ziara katika gridi ya taifa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Karemani, katika ziara hiyo amemtaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Abdallah Ikwasa kumuondoa kazini mtumishi huyo kwa madai kwamba amekuwa mzembe.

 “Leo meneja wa Kidatu sitaki kumsikia akiwa kwenye kazi nataka kuona nani umemuweka, lakini aondoke kwanza, na wewe protection nimekupa siku tatu kuhakikisha unarekebisha mfumo wako, tunataka mtuambie nini kimetokea nini tuzuie ili kisitokee, hatuwezi kufanya kazi kwa mazoea, huwezi ondoka na nawaambia leo umeme ukizimika nataka kukuta barua nyie wenyewe mmeacha kazi” amesema.

Tazama Video hapo chini…..

error: Content is protected !!