Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapato TRA 2015/17 yashuka kwa bilioni 100
Habari Mchanganyiko

Mapato TRA 2015/17 yashuka kwa bilioni 100

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo
Spread the love

KWA takribani miezi 23  tangu Rais John Magufuli aingie Ikulu, Mapato ya serikali kwa mwezi yameshuka kutoka trilioni 1.4  Desemba 2015  hadi kufikia Sh. 1.2 trilion mwezi uliopita, anaandika Angel Willium.

Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA),  imetoa taarifa ya makusanyo ya mapato kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018 katika kipindi cha mwezi  Julai hadi Septemba 2017.

Katika taarifa hiyo TRA imesema kati ya mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu, imekusanya mapato yanayofikia Sh. 3.65 trilioni.

Taarifa hiyo imesema kuwa mwezi Julai TRA ilikusanya Sh. 1.1 trilioni, Agosti Sh. 1.2 trilioni na  Septemba Sh. 1.3 trilioni.

Ukigawanya mapato hayo ni kama TRA imekusanya wastani wa Sh. 1.2 trilioni kwa mwezi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu ya Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema makusanyo  hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2016/2017.

Amesema kuwa kodi za hapa Tanzania zinatokana na viwanda,  ajira na kodi za bidhaa zinazotoka nje ya nchi.

“Wananchi wanatakiwa kukagua risiti zao kila wanapopewa ili waweze kuhakiki taarifa zilizoandikwa na kama ni halisi ili kudhibiti wakwepa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!