Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Nani kuibuka mshindi Liberia leo?
Kimataifa

Nani kuibuka mshindi Liberia leo?

George Weah, Mshindi wa Urais
Spread the love

WANANCHI nchini Liberia leo wanapiga kura kumchagua mrithi wa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika na mshindi wa tuzo la amani la Nobel, Ellen Johnson Sirleaf.

Aliyekuwa mcheza kandanda nyota George Weah, na makamu wa rais Joseph Boakai ndiyo wagombea wenye nguvu katika kinyang’anyiro

Liberia ni nchi iliyobuniwa na watumwa walioachiliwa huru kutoka Marekani karne ya 19, haijakuwa na mabadiliko ya amani ya madaraka kwa kipindi cha miaka 73.

Sirleaf aliwashauri watu kupiga kura kwa amani kwenye taifa hilo ambalo bado linajijenga kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14.

“Kura yako inakuhusu wewe na familia yako, sio chama wala kabila,” alisema Sirleaf wakati akihutubia taifa. Jumla ya wagombea 20 wa urais wanawania urais kumrithi Sirleaf.

Rais wa sasa mwenye umri wa miaka 78 anaondoka madarakani baada kuongoza kwa mihula miwili.

Aliingia madarakani mwaka 2006 baada ya mtangulizi wake Charles Taylor, kulazimishwa kuondoka madarakani na waasi mwaka 2003.

Taylor kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makosa yanayohusu uhalifu wa kivita na mzozo katika nchi jirani ya Sierra Leone.

Weah mwenye umri wa miaka 51, amemteua mke wa zamani wa Taylor Jewel Howard, kama mgombea mwenza.

Sirleaf ameshindwa kumfanyia kampeni Boakai na kuzua uvumi kuwa wawili hao huenda wametofautiana.
Karibu watu milioni 2.2 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!