Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamanda Msangi awekwa kitimoto Mwanza
Habari Mchanganyiko

Kamanda Msangi awekwa kitimoto Mwanza

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza
Spread the love

ZAIDI ya wakazi 23,000 wa mitaa 10 ya kata ya Pamba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, wameliomba jeshi la polisi kuwajengea uwezo na mbinu za kiitelenjensia wenyeviti wa Serikali za mitaa ili kuwabaini watu wanaojihusisha matukio ya uhalifu, anaandika Moses Mseti.

Pia wameomba jeshi hilo kuwajengea uwezo watendaji wa kata nchini ili na wao waweze kuwabaini wahalifu hao, kitendo ambacho kitasaidia kuondokana na matukio ya uhalifu ambayo yanaonekana kutishia usalama wa raia na mali zao.

Wananchi hao wametoa ombi hilo leo katika mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kuelezea kero za matukio ya uhalifu kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, kuhusu matukio yanayotokea katika mitaa yao.

Mmoja wa wananchi hao ambaye ni mkazi wa Bugarika, Hezron Bituro, amesema matukio ya uhalifu katika mitaa yao imekithiri hatua ambayo inahatarisha usalama wa raia na mali zao.

Amesema matukio ya unyang’anyi wa kutumia nguvu katika mitaa hiyo yameonekana kuongezeka kila kukicha hivyo jeshi hilo linapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwabaini wahalifu hao.

“Viongozi wetu wa serikali za mitaa na kata wajengewe uwezo wa kuwabaini watu ambao ni wahalifu, watu wanahamia kwenye mitaa bila taarifa ukiwauliza wanafanya kazi wapi wanajibh wanafanya kazi kwa muhindi kumbe ni wahalifu, lakini kama wangekiwa na uelewa wangekuwa wanawabaini mapema.

“Tunaomba pia kituo cha polisi cha Bugarika kwa sababu ndiyo imeonekana kama njia kuu ya majambazi wanapotoka hapa kueleke Buzuruga wanashindwa kushuka Igogo na Mabatini kwa sababu wanafahamu kuna vituo vya polisi ni vizuri na hapa tukawekewa kituo, ” amesema Bituro.

Mkuu wa polisi Wilaya ya Nyamagana, Mrakibu wa Polisi, Ochieng Asiago, alitumia nafasi hiyo kuwataka waendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda, kuepuka kubeba abiria wasiowafahamu hususani nyakati za usiku kwa tamaa ya fedha.

Akijibu kero mbalimbali ikiwemo za unyang’anyi wa kutumia nguvu na uporaji, kamanda Msangi, amesema jeshi hilo litaendelea kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao huku akiwataka wananchi hao kuwa walinzi namba moja katika maeneo yao.

Miezi sita iliyopita mkoa wa Mwanza hususani wilaya ya Nyamagana, matukio ya uhalifu na uporaji wa kutumia silaha za moto yalishamili kwa kasi na kusababisha watu zaidi ya 10 kupoteza maisha ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi chini ya Kamanda huyo wa Polisi, liliendesha msako mkali wa kuwasaka wahalifu hao na kufanikiwa kuwatia mbarano watu kadhaa na kuuawa majambazi takriabani 15 kwa kipindi hicho cha miezi mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!