MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa kupokea kielelezo cha nakala ya dawa anazozotumia mfanyabiashara, Yusuf Manji iliyotolewa na katibu muhtasi wake (sekretari), anaandika Faki Sosi.
Mahakama hiyo imeendelea kupokea vielelezo mbalimbali kama ushahidi chini ya hakimu, Cyprian Mkeha.
Wakili wa utetezi, Hajra Mungula alimuongoza shahidi Maria Rugalabumu ambaye amekuwa msaidizi wa Manji tangu mwaka 1994.
Shahidi huyo amedai kuwa yeye ndiye aliyetoa kopi ya nakala ya dawa za Manji kutoka kwa daktari wake wa Marekani ambazo zinadaiwa kuwa zina chembechembe za (Morphine).
Nakala hiyo aliipata kwa njia ya barua pepe (e-mail), ambapo baada ya kuitoa nakala alimpatia askari ili ampe Manji ambaye alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hivyo anaomba mahakama ipokee kama sehemu ya kielelezo.
Wakili wa serikali mkuu, Timony Vitalis alipinga kupokelewa kwa barua hiyo kwa sababu haina uthibitisho wa kiuhalisia na daktari aliyeituma.
Hakimu Mkeha alitoa uamuzi wa kutopokea kielelezo hicho cha nakala ya barua na kwamba amesema mahakama haiwezi kupokea kielelezo hicho.
Shahidi huyo amemfahamu Manji tangu anasoma chuo, hadi alipoanza kufanya kazi kwa Baba yake tangu 1997.
Shahidi huyo amesema kuwa amekuwa akitunza baadhi ya vitu vya Manji kama vile sigara na kwamba ameshangazwa kusikia bosi wake huyo ambaye yupo naye takribani miaka 19 kwamba anatumia dawa za kulevya.
Leave a comment