Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makubwa ya Yusuf Manji mahakamani
Habari MchanganyikoTangulizi

Makubwa ya Yusuf Manji mahakamani

Yusuf Manji
Spread the love

DAWA zinazotumikia kwenye matibabu ya ugonjwa wa moyo wa mfanyabiashara, Yusuf Manji zimezua mjadala kwenye ushahidi wa kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha upande wa utetezi ulileta mashahidi wake. Shahidi wa kwanza alikuwa mtuhumiwa mwenyewe Manji na kufuatiwa na Wakili wa utetezi.

Wakili wa utetezi Hajra Mungula ndiye aliyemuongoza shahidi wa kwanza ambaye alieleza kuwa dawa alizokuwa akitumia kwa matibabu zenye mchanganyiko wa (Morphine) ni za kupunguza makali ya maumivu ya ugonjwa unaomsumbua.

Manji alidai kuwa anatumia dawa hizo kwa maelekezo ya daktari wake na siyo vinginevyo.
Wakili wa Serikali, Thimon Vitalis alihoji matumizi ya dawa hizo alizokuwa akizitumia kwa kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) .

Mtuhumiwa alidai kuwa yeye anatumia kwa matumizi binafsi ya kijitibu na siyo biashara.
Wakati huo shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Daktari Bingwa wa Ugonjwa na Tiba ya Moyo kutoka Hospital ya Aga

Khan Professa Mustapha Babumia ambaye ni daktari anayemtibu. Amedai kuwa alimpokea Manji Tarehe Februali, 2 mwaka huu na kumfanyia vipimo vya kitalaamu na kugundua kuwa moyo wa mtuhumiwa huyo umeziba licha kufanyiwa upasuaji na matibabu ya kuziba sehemu tatu za moyo wake.

Amesema alibaini kuwa Manji kupata matibabu ya kuzibuliwa mara tatu sehemu za moyo zilizoziba nchini India, Marekani na Dubai.

Profesa Babumia alidai kuwa baada ya uchunguzi huo na maelezo ya mgonjwa walimpa dawa za kupunguza rehemu, kupunguza hofu na kupunguza maumivu ya mgongo kutokana na kugundua kusumbulia na matatizo hayo licha ya kumshauri wamfanyie upasuaji.

Alieleza kuwa dawa hizo huwezi kupewa bila ya uthibitisho wa daktari. Hata hivyo, jioni Manji alizidiwa na kurejeshwa hospitalini hapo na baadaye alikuwepo hapo kwa uangalizi kwa Siku 14.

Wakili alimuuliza kuhusu matumizi ya dawa zenye Mofon kunahusiana vipi na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua Manji.

Profesa Babumia alidai kuwa dawa hizo ni za maumivu na hutumika kwa wagonjwa wa Saratani na taasisi zinazoshughulikia magonjwa hayo kwa kibali ya Mamlaka.

Ameiambia mahakama kuwa dawa hizo zinatumika kwa wagonjwa wenye maumivu makali.

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!