Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mabalozi, mashirika ya kimataifa yapongeza tamasha la jinsia
Habari Mchanganyiko

Mabalozi, mashirika ya kimataifa yapongeza tamasha la jinsia

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan
Spread the love

BALOZI wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan amesema hakutakuwa na mafanikio bila utambuzi wa haki za makundi yaliyokandamizwa, anaadika Pendo Omary.

Gilsenan ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa maazimisho ya Tamasha la Jinsia linalowakutanisha wanaharakati zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Tamasha hilo la 14 limeandaliwa na TGNP-Mtandao kwa kushirikiana na Asasi mbalimbali.

“Tunasheherekea, lakini tunajua changamoto bado zipo. Ireland pia ukatili bado upo. Ujenzi wa vuguvugu la wanawake, kuwa na sera ni nyenzo muhimu sana katika kuleta usawa,” amesema Gilsenan.

Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini, Kayarina Rangnitt amesema anatambua mchango wa serikali ya Tanzania katika kufanya kazi ya kupigania usawa wa kijinsia.

“Nachoweza kusema, kwa siku hizi nne za tamasha la jinsia, litakuwa ni jukwaa la kushirikishana mafanikio, changamoto na nini kifanyeke katika kumkomboa mwanamkle na mtoto wa kike,” amesema Rangnitt.

Rangnitt amesema bado kuna kazi kubwa ya kumkomboa mtoto wa kike lakini wanaume wana wajibu wa kuunga mkono harakati hizo na hawapaswi kukimbia.

Aidha, Rangnitt amesema nchi yake ina ina mahusiano mazuri na TGNP- Mtandao kwa muda wa takribani miaka 20 hivyo anaupongeza kwa kuwa jukwaa huru la wanawake.

Pia, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women), Hodan Addou amesisitiza kuwa “Tunawapongeza TGNP lakini ipo kazi kubwa mbele yetu ya kumkomboa mwanamke na kujenga ushirika wa kusukuma gurudumu la maendeleo.”

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kitaifa wa Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Christina Mwanukuzi amesema “usawa sio kupika na kupakua. Upo katika hali ya utu wa mwanadamu.”

“UNFPA tunaunga jitihada za kumkomboa wanamke na mwanaume. Tunashirikiana na vijana pia,” amesema Mwanukuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!