Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TGNP yatoa tuzo kwa wanawake
Habari Mchanganyiko

TGNP yatoa tuzo kwa wanawake

Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania
Spread the love

TGNP Mtandao imetoa tuzo kwa wanawake waliojitoa kwa ajili ya kutetea wenzao hapa nchini na nje ya Tanzania anaandika Pendo Omary.

Akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanywa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Dr. Vincesia Shule ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao amesema wanawake wamekuwa chanzo cha mafanikio ya watu binafsi, taasisi mbalimbali na taifa kwa ujumla.

“TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji wa Kumbukumbu za wanawake nchini, kwa miaka mingi imekuwa ikiweka kumbukumbu za michango mbalimbali kwa kufanya tafiti juu ya maisha ya baadhi ya wanawake, kuandika hadithi za maisha yao na kuweka taarifa hizi katika tungo, picha , michoro na vitabu,” amesema Shule.

Wanawake waliopewa tuzo ni wanachama wa TGNP, Fides Chale (hayati), Prof. Marjorie Mbilinyi, Agripina Mosha, Mary Rusimbi, Demere Kitunga, Aseny Muro, Zippora Shekilango na Subira Kibiga.

Pia wamo Samia Suluhu, Theresia Mahagatila ( dereva wa treni wa kwanza nchini), Esther Bulaya, Mbunge wa jimbo la Bunda kwa jitihada zake za kupambana na mfumo dume katika nafasi za uongozi, Mwami Theresa Ntare wa IV (Mwanamke wa kwanza mwenyekiti wa baraza la machifu Tanzania) na Pili Hussein (mjomba Hussein) –mchimbaji wa kwanza mwanamke nchini.

Wengine ni Anna Makinda- Spika wa kwanza mwanamke wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Getrude Mongela ambaye ametoa mchango katika harakati za kusimamia na kupigania usawa wa kijinsia ndani na nje ya nchi, Anna Abdallah , Asha Rose Migiro, Thabitha Siwale, Ester Mwaikambo-dakatari wa kwanza mwanamke, Florah Mathias –mwanaharakati ngazi ya jamii na Fatuma Binti Baraka (hayati Bi. Kidude) ambaye alifanya harakati za ukombozi wa wanawake kwa kutumia muziki wa taarabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!