Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya madini kutua kwa Ndugai leo
Habari za Siasa

Ripoti ya madini kutua kwa Ndugai leo

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Job Ndugai leo atapokea ripoti mbili za tume maalum alizounda kwa ajili ya ushauri juu ya mfumo bora wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya Madini ya Almasi hapa Nchini, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa na Spika Ndugai alipokuwa akitoa matangazo kwa wabunge muda mfupi baada ya kumaliza kwa kipindi cha maswali na majibu jana Bungeni.

Ndugai amesema kuwa leo itakuwa siku ya tofauti kwani baada ya kipindi cha maswali na majibu atapokea ripoti hizo na kumkabidhi waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Nawashukuru wote wabunge kesho (leo), itakuwa siku ya tofauti sani kwani baada ya kipindi cha maswali na majibu nimemuomba Waziri Mkuu Masim Majaliwa awepo maana nitapokea taarifa za kamati kama mnavyujua nilizitangaza hapa bungeni na watanikabidhi na mimi nitamkabidhi Waziri Mkuu,” amesema Ndugai.

Spika wa Bunge aliunda kamati hizo Juni 30 mwaka huu kabla ya kuhitimisha shughuli za Bunge la Bajeti na kutoa siku 30 ili kamati hizo ziwe zimewasilisha ripoti hiyo.

Spika amesema ameunda kamati hiyo kupitia Waraka wa Spika namba 3 wa mwaka huu.

Awali Spika amesema kuwa Kamati hiyo itatathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Almasi nchini kisha kuandaa mapendekezo mahsusi kwa ajili ya kuishauri Serikali kuhusiana na uendeshaji bora wa biashara ya madini hayo nchini.

Amewataja wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni Mbunge wa Viti maalum(chadema) Dk. Immaculate Sware Semesi, Mbunge wa Viti maalum (CCM) Shally Raymond, Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdallah(CUF), Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula(CCM), Mbunge wa Viti maalum(CCM) Restituta Mbogo, Mbunge wa Wawi Ahmed Juma Ngwali(CUF).

Wengine ni Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa(CCM), Mbunge wa Tabora, mjini Emmanuel Mwakasaka(CCM) na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM) ambaye atakuwa Mwenyekiti.

Amesema wajumbe hao wameteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya taaluma, uzoefu, pande za Muungano, jinsia na uwakilishi wa Vyama vya Siasa bungeni.

“Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku thelathini kuanzia Julai 10, na Kituo Kikuu cha kazi kitakuwa katika Ofisi ya Bunge hapa Dodoma,” amesema.

Aidha, amesema hadidu za rejea za kamati hiyo zilikuwa ni taarifa za tue na kamati mbalimbali zilizowahi kuundwa na Serikali kwa ajili ya kushughulikia mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini na kuona Mapendekezo yake na namna yalivyotekelezwa na Serikali.

Nyingine ni Kutathmini mfumo uliopo wa uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa biashara ya madini ya almasi nchini na kubainisha manufaa ambayo Serikali inapata kutokana na uwekezaji uliopo katika madini hayo na kubainisha na kushauri kuhusu utaratibu bora unaoweza kutumika katika kusimamia uwekezaji, uchimbaji na biashara ya madini ya almasi nchini,” amesema Spika Ndugai

“Hadidu nyingine ni kushughulikia jambo jingine lolote linalohusiana na mfumo wa uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa madini ya almasi nchini,” amesema

Amesema kuundwa kwa Kamati hiyo kumetokana na pendekezo la Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli la kuunda Tume ya kuchunguza na kufuatilia madini ya alamasi alilolitoa Juni 12 mwaka huu alipohudhuria mkutano wa kupokea Taarifa ya Kamati yake ya Pili ya Kuchunguza Masuala ya Kiuchumi na Kisheria kuhusu Usafirishaji wa Makinikia, Kamati ya Prof. Nehemia Osoro).

Amesema Bunge liliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa kadri itakavyohitajika katika kuhakikisha kwamba juhudi, uthubutu na uzalendo aliouonesha Rais katika kulinda rasilimali za madini haupotei bure.

Hata hivyo, amesema kuundwa kwa Kamati hiyo ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa Azimio la Bunge la kumpongeza Rais Magufuli katika jitihada za kulinda rasilimali za Taifa.

“Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa madini ya almasi duniani, Madini haya yana thamani na umaarufu mkubwa katika biashara ya vito,kama ilivyo kwa dhahabu na madini mengine ya thamani, yapo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali nchini kwamba hatujaweza kunufaika ipasavyo kutokana na wingi na thamani ya madini ya almasi,” amesema Spika

Kamati hii itakayofuatilia kuhusu mfumo wa uchimbaji wa Madini ya Almasi hapa nchini ni ya pili kuudwa na Spika baada ya Kamati ile itayofuatilia suala la uchimbaji wa Madini ya Tanzanite hapa nchini ambayo pia aliuunda wakati wa mkutano wa Saba wa Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!