Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Veta yaanzisha kozi ya makanikia
ElimuHabari Mchanganyiko

Veta yaanzisha kozi ya makanikia

Yona Mwambopa, Mkufunzi wa Veta akizungumza na Mwandishi wa habari wa MwanaHALISI Online katika viwanja vya Sabasaba
Spread the love

CHUO cha Ufundi Stadi (VETA) kimeanzisha kozi itakayozalisha wahitimu watakaosaidia kuchakata na kung’arisha madini ya vito, anaandika Jovina Patrick.

Kozi hiyo inakuja kipindi ambacho hivi karibuni serikali imezuia kusafirisha mchanga wa madini (makinikia) nje ya nchi ili kuuchakata.

Akizungumza kuhusu kozi hiyo, Yona Mwambopa Mkufunzi wa Veta, amesema kozi hiyo kwa mara ya kwanza waliitambulisha miaka mitatu iliyopita ila ikakabiliwa na changamoto za kutokuwa na vitendea kazi vya ufundishaji.

“Kama tungekuwa na vifaa tayari tungekuwa tumeshazalisha wataalam wetu hapa hapa nchini,” amesema Mwambopa.

Mwambopa amesema kwamba mwaka huu wameanzisha tena kozi hii lakini muitikio sio wa kuridhisha.

“Hadi sasa tuna wanafunzi 12 ambao wapo chini ya kadirio la elimu nchini wakati inahitaji wanafunzi wasiopungua 16 na wasiyozidi 20,” amesema.

Amesema sababu ya muitiko kuwa mdogo umetokana na ugeni wa kozi hiyo wengi hawajafahamu faida zake, kwani Watanzania wengi wamekuwa wakisoma kozi baada ya kujua faida wanayopata baada ya kuhitimu.

Mwambopa anasema: “Naamini baada ya mafanikio yatakayopatikana kwa wahitimu hawa itawavutia wengine kujiunga zaidi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!