Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TRA kupiga mnada jengo la Star TV
Habari za SiasaTangulizi

TRA kupiga mnada jengo la Star TV

Anthony Diallo, Mmiliki wa Sahara Media ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,
Spread the love

KAMPUNI ya Sahara Media Group (SMG), inayomiliki kituo cha Televisheni Star tv, Redio Free Africa (RFA) na Kiss FM imefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushindwa kulipa kodi ya Sh. 4.5 bilioni, anaandika Irene Emmanuel.

Pia kampuni hiyo imepewa siku 14 (wiki mbili) kuanzia sasa, iwe imelipa kiasi hicho cha fedha na kama haitafanya hivyo majengo ya kampuni hiyo yatapigwa mnada ili kufidia deni hilo.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, inadaiwa kiasi hicho cha fedha za malimbikizo ya kodi ya kipindi cha awali huku kipindi cha miaka miwili 2016 – 2017 bado akiwa anadaiwa fedha ambazo hazijawekwa wazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Sukar Action Mart na Court Brokers, Lyasuka Sarehe, amesema kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya kampuni hiyo kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Salehe amesema kuwa kutokana na hali hiyo, wanachukua ya kuifunga huku wakitoa siku 14 kuanzia sasa, fedha hizo ziwe zimelipwa na kwamba kama haitafanya hivyo, watachukua hatua nyingine yakupiga mnada jengo hilo.

“Hizi siku 14 tulizotoa akishindwa kulipa tutaitisha mnada wa hadhara kwa ajili ya kukomboa kodi ya Serikali na kama kampuni isipolipa tutapiga mnada jengo hilo,” amesema Sarehe.

Madalali wa Sukar Action Mart na Court Brokers wakifunga ofisi za Sahara Media Mwanza

Ernest Dunde, Meneja wa TRA mkoani Mwanza, amesema kazi ya Serikali ni kukusanya kodi kwa mtu na kwa kampuni yeyote inayodaiwa na kwamba ni lazima deni hilo lilipwe hivyo zoezi la kukusanya madeni ni endelevu na yeyote anayedaiwa lazima atalipa.

Raphael Shilatu, Meneja wa Utumishi na Utawala wa kampuni ya Sahara Sahara, amesema ni kweli wamekuwa na malimbikizo ya kodi ya muda mrefu, huku akitaja sababu ni Serikali kuwataka kutoka analogia kwenda digitali.

“Hali hiyo ilitufanya kuyumba sana kiuchumi mara baada ya kufanya uwekezeji huo mkubwa tulijikuta tunayumba kiuchumi na kukaribisha madeni mengi na yaliyopelekea hali kama hii,” amesema Shilatu.

Shilatu pia aliwataka wapenzi na wasikilizaji wa vyombo hivyo kuwa na moyo wa uvumilivu na kwamba kipindi hiki ni cha mpito mambo yatakuwa sawa na hakuna jambo litakalo haribika.

Kabla ya zoezi la kufunga geti za kampuni, wafanyakazi wa kampuni walionekama kupigwa na butwaa na wengi wao wakianza kuondoa magari yao nje ya geti ili yasifungiwe ndani kama gari za kampuni ambazo zimefungiwa ndani.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!