
Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP)
SIMON Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) amefanya mabadiliko ya kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani pamoja na kamanda wa polisi wa mkoani Mbeya, anaandika Irene David.
Katika mabadiliko hayo, Mohamed Mpinga, aliyekuwa Kamanda wa polisi kikosi cha usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa polisi amehamishwa na kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.
Aidha nafasi yake inachukuliwa na Fortunatus Musilimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi (SACP), aliyekuwa Kamanda wa polisi Mkoani humo (DCP) Dhahiri Kidavashari ameamishwa Makao Makuu ya upelelezi.
IGP Sirro amesema mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi nchini.
More Stories
Mpogoro ahamasisha sensa
Wafugaji nyuki watakiwa kutumia zana za kisasa
Muarobaini kumuokoa mkulima na wadudu