Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani CUF ‘wamzodoa’ Lipumba
Habari za Siasa

Madiwani CUF ‘wamzodoa’ Lipumba

Spread the love

JUMLA ya madiwani 19 kati ya 21 wa Chama cha Wananchi (CUF), katika jiji la Dar es Salaam, wameunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na usajili  wa bodi mpya ya udhamini wa chama hicho, anaandika Catherine Kayombo.

Akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika katika ofisi za  CUF   Magomeni, Musa Kafana  mwakilishi wa madiwani hao ambaye pia ni naibu meya wa jiji la Dar es Salaam amesema kuwa wanapinga na kulaani vikali vitendo vya kukivuruga chama hicho vinavyofanywa na aliyekua mwenyekiti wa CUF Profesa  Ibrahim Lipumba.

“Tunapinga juhudi zinazofanywa na Prof. Lipumba na wafuasi wake wote ambao wamekua na vitendo na mwenendo usiofaa, wa kuharibu mali za chama, kuiba fedha za ruzuku, kusababisha uvunjifu wa amani na kuharibu taswira ya chama mbele ya jamii,” amesema Kafana.

Naibu meya huyo amelaani njama na mipango ya Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa kumtambua na kuwataka wana CUF wamrudishe Lipumba katika nafasi ya uenyekiti kwa madai alitengua barua yake ya kujiuzulu.

“Si Jaji Mutungi wala Profesa Lipumba aliyeweza mpaka leo hii kuwaeleza wana CUF na watanzania kwa ujumla ni Ibara ipi ya katiba ya CUF inayoruhusu kiongozi akijiuzulu anayo haki ya kutengua kujiuzulu kwake kwa kumuandikia barua katibu wa mamlaka iliyomchagua,” amesema.

Kafana amesema madiwani wa CUF pia wanapinga na kulaani kitendo cha Mamlaka ya usajili wa vizazi na vifo – RITA  kwa uamuzi wake wa kusajili majina ya wajumbe wapya wa bodi ya udhamini ya CUFkinyume na kifungu cha 26 cha sheria ya wadhamini (The Trustees’ Incorporation Act  Cap. 318).

“Tunaungana na pendekezo la chama cha kuwakilisha maombi mbele ya mahakama kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote zilizofunguliwa na chama kuhusiana na kadhia hii hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya Rita litakapoamuliwa.”

Aidha, madiwani hao wamelaani pia hatua ya Ally Happi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuamuru Halima Mdee, Mbunge wa Kawe awekwe rumande masaa 48 kwa tuhuma ya kumkashifu Rais John Magufuli.

“Halima Mdee ni sehemu ya madiwani katika jiji la Dar es Salaam, lakini pia ni Mjumbe wa baraza la jiji. Sisi chama cha Wananchi – CUF tunalaani kitendo hiki kwasababu tunaona ni ukiukwaji wa haki za binadamu maana kila mtu ana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake,” amesisitiza Kafana.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!