Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC mwingine wa Rais Magufuli ajiuzuru
Habari za Siasa

DC mwingine wa Rais Magufuli ajiuzuru

Spread the love

DK. Leonard Masale, Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo kwa hiari yake mwenyewe baada ya kumwandikia barua Rais John Magufuli barua ya kuachia ngazi katika nafasi hiyo, anaandika Moses Mseti.

DK. Masale anakuwa ni mkuu wa wilaya wa pili kuachia ngazi baada ya Januari 26 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Mnyele kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa hiari yake kwa kumwandikia rais John Magufuli barua ya kuomba kuachia ngazi.

DC Mnyele ambae wakati anaondoka katika nafasi hiyo, alipata fursa ya kuwaaga makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ofisi za CCM, Wilaya ya Uyui ambao walikuwa wakifanya mkutano wa kawaida hasa madiwani wa chama hicho ambao walikuwa wakijiandaa na kikao cha Baraza la Madiwani la Wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela ambaye alimwandikia rais barua ya kuachia ngazi Julai 4 mwaka huu, kwa madai kwamba amefikia umri wa kustaafu kama taratibu za utumishi wa umma zinavyoelekeza kwamba mtumishi wa umma anapofikia umri wa 60 anapaswa kustaafu utumishi.

Pia inaelezwa kwamba mkuu huyo wa wilaya, ameshindwa kuendana na kasi ya rais John Magufuli huku akituhumiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kusababisha kulazimishwa kuachia ngazi kwa hiari yake mwenyewe.

Chanzo kutoka ndani ya ofisi ya mkuu huyo wa wilaya, kinasema kwamba, kwa kipindi kirefu viongozi wakuu wa mkoa na ngazi za juu, walikuwa wakimshinikiza kuachia nafasi hiyo kitendo ambacho kimemlazimu kuchukua maamuzi magumu.

Akizungumza na mtandao huu leo, mkuu huyo wa wilaya amesema amelazimika kuandika barua ya kubwaga manyanga kutokana na umri wake kufikia wa kustaafu kufikia huku akidai tayari ameshalipwa mafao yake ya kustaafu utumishi wa umma.

“Watumishi wa Serikali wakifikisha umri wa miaka 60 ni wajibu wao wa kustaafu. Kabla ya kufikia tarehe ya kustaafu, mtumishi anatakiwa kuandika barua miezi sita kabla ya tarehe hiyo ili taasisi zinazoandaa mafao yao waweze kumwandalia mafao yake miezi miwili kabla.

“Pia na mimi nimefikia umri huo na nimelipwa mafao na pensheni yangu na PSPF, hivyo hivi sasa mimi ni raia mwema wa nchi hii ila nikiteuliwa kufanya kazi yoyote ile nina uwezo wa kuchapa kazi,” amesema Dk. Masale.

Mtandao Huu, ulipomtafuta Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, kutaka kufahamu kama tayari amepokea barua ya kiongozi huyo kujiuzuru, amekiri ni kweli amepokea barua lakini hakuwa tayari kuweka wazi siku aliyoipokea.

Mongella amesema kuwa alipokea barua ya mkuu huyo wa wilaya, akimtaarifu kwamba ameamua kuachia nafasi hiyo kwa kuwa umri wake wa kustaafu umefika huku Mongella akidai yeye ameipokea barua hiyo na wenye mamlaka ya kulizungumzia zaidi ni mamlaka zilizomteua.

Dk. Masale amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji katika halmashauli tatu ambazo ni Halmashauli ya Wilaya ya Ukerewe (Mwanza), Halmashauli ya Itilima (Simiyu) na Halmashauli ya Busokelo mkoani Mbeya katika kipindi cha mwaka 2005 – 2010.

Hata hivyo, baada ya mkuu huyo wa wilaya kuachia ngazi, ofisi hiyo hivi sasa inakaimiwa na mkuu wa wilaya ya Magu, Khadija Nyembo, kwa kuwa ndiye DC mwenye uzoefu wa nafasi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!