Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli awakingia kifua Mkapa, Kikwete sakata la madini
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli awakingia kifua Mkapa, Kikwete sakata la madini

Kutoka kushoto, Rais John Magufuli, Wastaafu Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa wakifurahia jambo walipokutana Ikulu
Spread the love

JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania amevijia juu vyombo vya habari vinavyowataja na kuwahusisha marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kwenye ripoti ya mikabata ya madini ya michanga wa dhahabu (Maknikia), anaandika Hamisi Mguta.

Ameyasema hayo leo kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa muda mchache baada ya kufanya mazungumzo na Prof. John Thornton, Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya ACACIA Mining Limited.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, walifanya kazi kubwa kulitumikia taifa letu, viwaache wapunzike,” amesema rais Magufuli.

Baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo ya pili, Marais hao wastaafu wamekuwa wakihusishwa kwenye sakata hilo la madini hasa kusainiwa kwa mikataba hiyo ya madini.

Marais hao wastaafu pia wametajwa bungeni kwa madai kuwa hawawezi kuwa salama katika sakata hilo kwani haiwezekani mawaziri wakuu wapitishe bila ya idhini ya viongozi wao wakuu.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema katika mazungumzo yake na Prof. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Katika taarifa nyingine, Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema baada ya rais kupokea ripoti ya mchanga wa dhahabu baadhi ya vyombo vya habari vimechukua fursa hiyo kurusha kila aina ya tuhuma kwa marais wastaafu.

“Ikumbukwe kwamba taarifa iliyotolewa na Kamati haikuwataja wala kuwatuhumu marais hao wastaafu, naviasa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuacha mara moja muelekeo huo hasi ambao unakila dalili ya kupotosha kampeni tuliyonayo ya kujikomboa kiuchumi,” amesema Mwakyembe.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!