Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halima Mdee kuliburuza Bunge mahakamani
Habari za Siasa

Halima Mdee kuliburuza Bunge mahakamani

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe
Spread the love

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee amesema wanatarajia kwenda mahakamani kwa ajili ya kupinga uamuzi wa Bunge wa kuwasimamisha kwa kutohudhuria vikao vya bunge kwa mwaka, anaandika Dany Tibason.

Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya, kwa madai ya kuwa wabunge hao wamevunja kanuni za Bunge kwa utovu wa nidhamu.
Mdee ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi juu ya matatizo makubwa yaliyopo katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2017/18.
Amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwani mahakama ni muhimili ambao unatoa haki hivyo anaamini haki itatendeka.
Juni 5, mwaka huu Mbunge  wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini  Esther Bulaya  walisimamishwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 ambapo hukumu hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi wa CCM kutokana na hoja ya mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza.

1 Comment

  • Tunakutakia kila la kheri! Hata hivyo tunashukuru kwamba bunge halioneshwi mbashara kwani vituko vyenu vinatia aibu! Acha tuwe tunawasikiliza tu kwenye redio!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!