Saturday , 10 June 2023
Habari za Siasa

Mdee airarua Bajeti

Spread the love

HALIMA James Mdee, Waziri kivuli wa Fedha na Mipango, na Mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), amechambua mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/2018, na kusema inalenga kuendeleza unyonyaji kwa wananchi, anaandika Dany Tibason.

Mapendekezo ya bajeti hiyo yaliwasilishwa bungeni Ijumaa iliyopita na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Uchumi, ambapo pamoja na mambo mengine serikali ilipendekeza kufuta ushuru wa leseni ya magari ya kila mwaka (Motor vehicle Raod licence) kwa wamiliki wa magari hayo na kuhamishia tozo hiyo katika mafuta ya petroli, dizeli na taa.

Mdee ambaye kwa sasa anatumikia adhabu inayomlazimu kutohudhuria
mikutano mitatu ya bunge, amewambia wanahabari mjini Dodoma kuwa bajeti ya kambi hiyo itawasilishwa leo na Joseph Silinde, Mbunge wa Momba ambaye ndiye Naibu Waziri Kivuli wa Wizara hiyo.

“Katika bajeti inayomalizika Juni mwaka huu, serikali ilitekeleza miradi ya maendelea kwa asilimia chini ya 40 tu, kwa kuwa fedha zilizotyajwa kuwa zoitatumika hazikuwepo. Ndivyo itakavyokuwa hata katika bajeti ya mwaka huu.

“Vyanzo vingi vya mapato ambavyo vilikuwa tegemeo kwa halmashauri, vimerejeshwa Serikali Kuu. Walisema kuwa sehemu
ya mapato hayo yatarejeshwa kwa halmashauri lakini haitendeki hivyo,”
amesema.

Kuhusu kufutwa kwa kodi ya ya leseni za gari, Mdee, alisema hiyo ni njia nyingine ya serikali kunyonya mwananchi kwani kodi hiyo imehamishiwa kwenye nishati ya mafuta, ikiwemo mafuta ya taa, ilihali vyombo vya moto havitumii mafuta ya taa.

“Hata mwananchi anayeishi kwa kutegemea vibatari ili kupata mwanga kwenye makazi yake, atalazimika kulipa kodi hiyo ambayo serikali imeipachika kwenyemafuta.

“Hata hao wamiliki wa magari wanaoshangilia, hawajapunguziwa mzigo kwa kiwango chochote bali wameongezewa, wajiulize wanatumia lita ngapi za petroli au dizeli kwa mwaka kisha wazidishe mara Sh. 40/- kwa kila lita,” amesema Mdee.

Aidha Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwansheria amesema, anashangazwa na kitendo cha serikali kutaka kila nyumba ambayo
haijafanyiwa uthamini itozwe Sh.10,000/- badala ya kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili watu wengi zaidi wajenge nyumba bora.

Ameeleza kuwa mapendekezo ya bajeti mbadala ya kambi ya upinzani yameibua vyanzo mbadala vya mapato ikiwemo uvuvi katika bahari kuu, sekta ya madini – vito, na  kupunguza misamaha ya kodi hadi
kufikia asilimia 1 ya pato la taifa.

“Vipaumbele vya bajeti mbadala kwa mchanganuo wa asilimia ni sekta ya elimu (20%), viwanda (15%), nishati (15%), kilimo (10%) na sekta nyinginezo ambazozimepatiwa asilimia 40 ya bajeti ya maendeleo.

“Vipaumbele hivi vikitekelezwa kwa ukamilifu, vitachochea ajira kwa
wengi na hivyo kupunguza umaskini kwa asilimia 50,” amesema Mdee.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!