August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halima Mdee kuliburuza Bunge mahakamani

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe

Spread the love

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee amesema wanatarajia kwenda mahakamani kwa ajili ya kupinga uamuzi wa Bunge wa kuwasimamisha kwa kutohudhuria vikao vya bunge kwa mwaka, anaandika Dany Tibason.

Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya, kwa madai ya kuwa wabunge hao wamevunja kanuni za Bunge kwa utovu wa nidhamu.
Mdee ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi juu ya matatizo makubwa yaliyopo katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2017/18.
Amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwani mahakama ni muhimili ambao unatoa haki hivyo anaamini haki itatendeka.
Juni 5, mwaka huu Mbunge  wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini  Esther Bulaya  walisimamishwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 ambapo hukumu hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi wa CCM kutokana na hoja ya mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza.
error: Content is protected !!