Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bavicha wamlaani Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Bavicha wamlaani Ndugai

Job Ndugai,. Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kumtoa kwa nguvu Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, John Mnyika, Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), limeaalani  kitendo hicho cha udhalilishaji kilichofanywa na  Spika, anaandika Hamisi Mguta.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba aliamuliwa jana kutoka nje ya Bunge na kutohudhuria vikao saba vya bunge vinavyoendelea kutokana na kilichoitwa na spika kuwa ni utovu wa nidhamu uliofanywa na Mnyika kwa kubishana na kiti baada ya kutokea malumbano kati yake na spika.

Patrobas Katabi, Mwenyekiti wa Bavicha, akizungumza na wanahabari leo katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni ameeleza kuwa Ndugai hakutumia busara kumtoa Mnyika bali alikuwa na jazba katika kutoa uamuzi huo.

“Tunasikitika na kitendo kilichofanywa na Ndugai, nadhani busara alizisahau nyumbani basi angejaribu hata kuzikumbuka kuliko kutoa uamuzi kama ule.

“Adhabu ya Mnyika kutoka nje ya Bunge ilitosha kabisa. Lakini si kumwambia asihudhurie vikao kwa siku kadhaa, ni wakati muafaka wa Ndugai kufanya upya marejeo ya uamuzi aliyoutoa ambao anadai ulikuwa wa jazba kuliko busara,” amesema Katambi.

Katambi amesema vita ya madini haiwezi kufanikiwa kwa kuwatoa  wapinzani nje ya Bunge ambao wana mawazo mbadala ambayo yanaweza kuwasaidia kwa namna moja au nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!