Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakwepa kodi 310 waburuzwa kortini
Habari Mchanganyiko

Wakwepa kodi 310 waburuzwa kortini

Taswila ya jiji la Mwanza
Spread the love

OFISI ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa, imewafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi 310, walioshindwa kulipa kodi hiyo kwa kipindi cha mwaka huu, anaandika Moses Mseti.

Wadaiwa hao wa kodi waliofikishwa kortini, pia imekihusisha Chama Kikuu cha Ushirika kanda ya ziwa (NCU) ambacho kwa sasa kinakumbwa na ukata wa kifedha pamoja na wafanyabiashara mbalimbali jijini Mwanza.

Wadaiwa hao 310 wamefikishwa katika baraza la ardhi na nyumba la Mwanza, wakidaiwa jumla ya kodi ya Sh. 2.2 bilioni ikiwa ni kodi ya mwaka huu pekee kwa kushindwa kulipia viwanja vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Ardhi Mteule anayeshughulika na masuala kodi ya ardhi, Elia Kamihanda, amesema kuwa wanapeleka wamiliki hao wa ardhi kuiomba mahakama kulipwa fedha hizo.

Kamihanda amesema pamoja na kuiomba mahakama kwamba wamiliki wa viwanja hivyo kuwalipa kodi pia amedai watakaoshindwa kulipa wataiomba mahakama wataifishe viwanja hivyo ikiwemo kufuta hatimiliki.

“Mwaka jana tuliwafikisha watu 150 mahakamani na tulikamata vitu vinavyohamishika na kutaifisha viwanja hivyo na kufanikiwa kupata kiasi cha Sh. 7.2 bilioni na lengo letu mwaka huu kwa idadi hiyo ya watu tutafikisha Sh. 11 bilioni.

“Tumeanza na Halmashauri mbili za Ilemela na Jiji la Mwanza na tutaendelea katika halmashauri zote 37 za kanda ya ziwa na mmiliki yeyote wa ardhi lazima alipe kodi ya ardhi na suala hili sio ombi ni lazima kwani lipo kisheria,” amesema Kamihanda.

Kamishna huyo msaidizi, amesema kuwa wamiliki wengi wamekuwa wakishindwa kulipa kodi ya ardhi kwa mujibu wa ardhi, kitendo ambacho kinaipelekea mamlaka hiyo kuchukua hatua kuwafikisha mahakamani.

Mmoja wa wadaiwa wa kodi, Chacha Marwa, alidai kwamba anashangaa kuona wakitakiwa kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kulipa kodi jambo kwake sio la kweli huku akidai kwamba yeye hadaiwi fedha yeyote.

“Hawa wanaotuleta mahakamani, wanasema mimi nadaiwa zaidi ya Sh. 1, 000, 000, siyo kweli, mimi sidaiwa fedha yeyote, kwanza hawatunzi kumbukumbu kuna siku ambayo nilienda kulipa kodi waliniomba baadhi ya nyaraka nilizowahi kulipa,” amesema Marwa.

Hivi karibuni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi, aliagazia ofisi hiyo kuwachukulia hatua za kisheria wadaiwa sugu wa ardhi wanaoshindwa kulipa kodi hiyo na kuisababishia hasara Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!