August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea, Mdee huru kesi ya kumshika matiti RAS

Washtakiwa wa kesi ya kumjeruhi RAS wa Dar es Salaam, wakiwa nje ya mahakama baada ya kuachiwa huru

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge wa Ukawa na madiwani wawili waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando katika uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam, anaandika Hamisi Mguta.

Wabunge waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo ni, Saed Kubenea (Ubungo), Halima Mdee (Kawe) na Mwita Waitara wa Ukonga.

Madiwani ni wa kata ya Kimanga, Manase Mjema, wa Saranga, Ephraim Kinyafu na kada wa chama hicho, Rafii Juma.

Washitakiwa hao wameachiwa huru leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata  mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.

Ushahidi wake ulielezea jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.

Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema: “Sijui alishikwa matiti na nani?” hivyo kutokana na  ushahidi huo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.

error: Content is protected !!