Friday , 24 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM mdaiwa sugu
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge CCM mdaiwa sugu

Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga (CCM)
Spread the love

JUMANNE Kishimba, Mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga (CCM) anatuhumiwa kushindwa kulipa kodi ya ardhi kiasi cha Sh. 2.7 milioni kwa kipindi cha mwaka huu, anaandika Moses Mseti.

Mbunge huyo anatuhumiwa kushindwa kulipa kodi hiyo ya fedha za kiwanja chake kilichopo Kapripointi na kingine cha Mjini Kati mkoani Mwanza, jambo ambalo linasababisha serikali kukosa mapato.

Pamoja na Kishimba pia mashirika na taasisi nyingine za serikali zinazodaiwa kushindwa kulipa kodi ni pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRL) kiasi cha milioni 10, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), milioni 18.2 na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) milioni 21.5.

Akizungunza na waandishi wa habari Afisa Ardhi Mteule anayeshughulika na masuala ya kodi, Elia Kamihanda, amesema kuwa mbunge huyo anadaiwa kiasi hicho cha fedha kwa kushindwa kulipia kiwanja chake namba 92 kilichopo Kapripointi jijini hapa.

Amesema kuwa mbunge huyo wa CCM na baadhi ya taasisi za serikali zimekuwa zikivunja sheria ya ardhi kwa kushindwa kulipa kodi kwa wakati jambo ambalo alidai linasababisha serikali kukosa mapato ya ardhi.

Kamihanda amesema wamedhamilia kuhakikisha kila mtu anayemiliki ardhi analipa kodi na kwamba hawatamuonea aibu mtu atakayeshindwa kutekeleza sheria kwa kulipa kodi kwa mujibu wa kanuni, taratibu za sheria zilizopo.

“Sasa hivi baada ya kusikia kwamba tumeanza kuwapeleka wafanyabiashara na watu wengine baraza la ardhi na nyumba kwa lengo la kuiomba mahakama kutupatia madalali kutaifisha mali zao kuna wengine wameanza kulipa akiwemo yeye (Jumanne Kishimba),” amesema Kamihanda.

Kamihanda amesema kuwa hawata muonea mtu aibu atakaenda kulipa kodi ya ardhi na kwamba atakaeshindwa kuanza kulipa kuanzia watataifisha mali zao zinazohamishika.

Pia amesema taasisi za serikali zimekuwa kikwazo kikubwa katika ulipaji wa kodi ya ardhi huku akitaja kampuni nyingine zilizofikishwa kortini kwa kushindwa kulipa fedha ni pamoja na Nsagali Oil Mill wanaodaiwa Sh. 13.9 milioni.

Kampuni Nyingine zinazodaiwa fedha hizo ni kampuni ya Bia ya Serengeti kiasi cha Sh. 32 milioni, Kampuni ya Nyakato Streel inayojihusisha na utengenezaji wa Nondo kiasi cha Sh. 10,130, 702.40 na kampuni ya mafuta ya GBP.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Serikali mbili ni sera ya CCM, si mkataba wa Muungano

Spread the loveMUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar uliotimiza miaka 60 tangu...

error: Content is protected !!