Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Uhaba wa dawa wakithiri Nyamagana
AfyaHabari Mchanganyiko

Uhaba wa dawa wakithiri Nyamagana

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Spread the love

UHABA wa dawa katika Hospitali ya wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, umezidi kuongezeka na kuwa kero kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma kwenye hospitali hiyo, kitendo kinachosababisha watu kupoteza maisha, anaandika Moses Mseti.

Miezi michache iliyopita zaidi ya watu wanane walipoteza maisha hospitalini hapo, kutokana na ukosefu wa dawa pamoja na uzembe wa wauguzi kitendo kilichosababisha baadhi ya wauguzi kusimamishwa kazi.

Miongoni mwa dawa ambazo hazipatikani hospitalini hapo ni Asprin, Parnadol na decofanace, huku baadhi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo hulazimika kwenda kununua katika maduka ya watu binafsi kitendo ambacho kimeonekana kero kwao.

Uhaba huo ulifahamika, baada ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kufanya ziara hospitalini hapo na kukuta ndugu wa wagonjwa walioandikiwa dawa za huduma ya kwanza ikiwemo Aspirin na Parnadol zikiwa hazipo.

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amesema kuwa, Mganga Mkuu wa Jiji hilo, Dk. John Andrew na wauguzi wake wamekuwa wazembe kwa kushindwa kuieleza mamlaka husika changamoto zinazoikabili hospitali hiyo na kusababisha vifo kwa wananchi.

Mongella amesema kuwa, vifo vya watu katika hospitali hiyo ya serikali imeonekana ni utamaduni wa kawaida, kwani baadhi ya wauguzi wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo huku hospitali hiyo inayotegemewa na wananchi wengi kutoaminiwa.

“Uzembe, usimamizi na utendaji wa hovyo na udhaifu wa uongozi wa hospitali hii ya serikali ndio chanzo cha watu kupoteza maisha na wauguzi wengine wanafanya kazi kwa mazoea na kufanya kile wao wanachotaka, hatuwezi kuendelea kuwa na hospitali hii.

“DMO (mganga mkuu wa jiji) na wewe umezidi ustaraabu haiwezekani changamoto nyingi zilizopo katika hospitali hii, umeshindwa kuchukua hatua, mpaka sisi tunafika hapa ndio tunaelezwa hizi changamoto haiwezekani nyie kuendelea kuwa hapa,” amesema Mongella.

Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, amesema kuwa, baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo, hazifahamu huku akidai kwamba tayari serikali ilitoa Sh. 80 milioni kwa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) kwa ajili ya kununua dawa hizo.

Kibamba amesema kuwa, Sh. 80 milioni zilizotolewa kwa ajili ya kupewa dawa, lakini hazikutolewa dawa zote na badala yake walipewa za Sh. 20 milioni kitendo ambacho kimechangia kuwepo na uhaba wa dawa hizo huku akiahidi kulighulikia kikamilifu.

Dk. John Andrew, Mganga Mkuu wa Jiji, amesema kuwa, pamoja na ukosefu wa dawa hizo lakini kuna dawa nyingine zinazopatikana hospitali hapo, huku akidai chanzo kilichochangia kukosekana kwa baadhi ya dawa hizo ni MSD kuchelewesha dawa zilizolipiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!