Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Mdee matatani, wapinzani wasusia bunge
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Mdee matatani, wapinzani wasusia bunge

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe akitoa mchango wake bungeni. Picha ndogo wabunge wa upinzani wakitoka bungeni
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, amewatia matatazi Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa makosa ya kutoa lugha ya matusi juzi katika uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA), anaandika Mwandishi Wetu.

Ndugai amemtaka Mbowe kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge leo ili kujibu tuhuma za kutoa matusi katika kikao cha bunge juzi wakati wa uchaguzi huo, na anatakiwa kufanya hivyo bila kukosa.

Mdee amepewa masaa 24 afike katika ofisi za bunge kujibu tuhuma za kumtukana Spika wa Bunge na asipofanya hivyo atawaagiza polisi wamkamate popote atakapokuwa na kumleta katia ofisi za bunge kwa nguvu.

Ndugai alitoa maagizo hayo leo asubuhi katika kikao cha Bunge la 11 mkutano wa saba, na kuwataka watuhumi hao kutekeleza maagizo hayo mara moja bila kukosa.

Katika hatua nyingine, wabunge wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge baada ya kupinga kupewa muda mdogo wa kupitisha miswada miwili ya sheria za mafuta na gezi.

Wabunge hao wametoka bungeni wakishinikiza kuongezewa muda uliopangwa na spika kitu ambacho wao wamepingana nao kwa madai kuwa ni mdogo kujadili mambo nyeti kama hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!