Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Kampuni ya Chai Kagera yakumbwa na ukata
Habari Mchanganyiko

Kampuni ya Chai Kagera yakumbwa na ukata

Shamba la chai Kagera
Spread the love

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imetaja kuwa ucheleweshaji wa malipo ya wakulima na wafanyakazi katika kiwanda cha chai cha Maruku mkoani Kagera ulianza Septemba, 2011 kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Kagera Tea Company Ltd, anaandika Dany Tibason.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, William Ole Nasha alitoa kauli hiyo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba (CCM), Jasson Rweikiza.

Rweikiza alitaka kujua ni kwanini serikali haichukui hatua ya kuwasaidia wakulima na wafanyakazi ili wapate haki yao ambayo wamekuwa wakiitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Kampuni ya chai ya Maruku imekuwa sugu kwa kutowalipa wakulima wanaoiuzia chai pamoja na kutowalipa wafanyakazi wake wenyewe,” amesema mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri amesema kutolipwa kwa wakulima na wafanyakazi hao kulitokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Kagera Tea Ltd iliyowekwa na Spearshield Africa Company Ltd anayemiliki kiwanda cha chai cha Maruku.

Alibainisha kuwa anamiliki kwa asilimia 75 katika kusimamia uendeshaji wake ikiwemo ununuzi wa majani mabichi ya chai kutoka kwa wakulima wadogo huku wakulima hao wakimiliki asilimia 25 walizopewa na serikali kufuatia kiwanda hicho kubinafsishwa kwa Spearshield Africa Company Ltd toka kwa mamlaka ya chai Tanzania waliokuwa wanamiliki kiwanda hicho.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni tija ndogo ya majani ya chai ikilinganishwa na gharama za uzalishaji lakini akasema serikali kupitia uongozi wa mkoa wa Kagera, Bodi ya Chai Tanzania na wakala wa wakulima wadogo wa chai Tanzania kwa nyakati tofauti walikutana na mwekezaji huyo kumwelekeza atekeleze wajibu wake wa kulipa wakulima na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Ole Nasha, kufuatia mikutano hiyo mwekezaji ametafuta fedha na kulipa madeni mbalimbali ikiwemo malimbikizo yote ya nyuma hadi mwezi Oktoba 2016 na ameahidi kulipa madeni ya Novemba Desemba 2016 ndani ya Januari 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!