Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bulembo atangaza kung’atuka CCM
Habari za Siasa

Bulembo atangaza kung’atuka CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo
Spread the love

ALHAJI Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ametangaza kung’atuka rasmi katika nafasi yake, kwa mdai kuwa anahitaji kuumzika, anaandika Dany Tibson.

Bulembo ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mbunge na Rais John Magufuli amesema hana mpango wa kugombea nafasi yoyote ndani ya CCM katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaofanyika mwaka huu.

Ametoa kauli hiyo katika baraza la dharura la jumuiya ya wazazi wa CCM kilichohudhuriwa na wajumbe 102.

“Si kwamba sina uwezo wa kugombea tena, ila tu nimeamua kupumzika na nikatulie kijiji  kwangu huku nikiendeleza shughuli nyingine.

“Msidhani kwamba nang’atuka kutokana na ubunge niliochaguliwa. Hapana, mimi ni mbunge ambaye jimbo langu ni Ikulu,” amesema.

Amesema ni wakati wa wajumbe wengine kutoka ndani ya jumuiya hiyo kuchangamkia fursa ya kugombea nafasi hiyo ya uwenyekiti bila kutegemea kubebwa na mtu yoyote.

“Msitegemee kuwa nitampigia mtu kampeni, nendeni mkachukue fomu ya kugombea kama mmejipima na kuona mna uwezo na asije mtu yoyote akasikika huko akiwadanganya kuwa ameongea na mimi na kwamba nitamuunga mkono katika uchaguzi,” amesisitiza.

Bulembo amedai kuwa mwanzoni Jumuiya ya wazazi ya CCM ilikuwa na wakati mgumu lakini yeye kama mwenyekiti kwa kushirikiana na viongozi wengine waliamua kufanya kazi ya kuiweka mahali mazuri jumuiya hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!