August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pombe za viroba, bangi zazua balaa Morogoro

Pombe zilizofungashwa katika mifuko ya nailoni maarufu kama Kiroba

Spread the love

OPERESHENI ya kukamata pombe ambazo hufungwa katika vifuko maalum maarufu kama viroba, imeendelea kushika kasi mkoani Morogoro ambapo sasa jeshi la polisi limewakamata jumla ya wafanyabiashara 14 waliokutwa na pombe hizo, anaandika Christina Haule.

Watu hao 14 wanatuhumiwa kukutwa na pombe kali za Viroba katoni 128, dazeni 11, pakiti 16 na vifungashio 7 katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro.

Urlich Matei, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro amesema polisi walianza operesheni dhidi ya pombe kali za vifungashio vya plastiki maarufu kwa jina la Viroba tarehe 3 Machi mwaka huu.

“Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao katika maeneo mbalimbali ya mkoa, wakiwa na viroba vya aina mbalimbali zikiwemo Value, Zed, Nguvu Spirit, Kiroba Original, Konyagi na Vodka.

“Watuhumiwa tuliowakamata wanaendelea kuhojiwa na polisi huku hatua za kuwafikisha mahakamani zikiendelea,” amesema.

Kamanda Matei pia ametangaza kuwa jeshi hilo linawashikilia watu wengine 16 kwa kukamatwa na bangi katika kijiji cha Singisa wilayani Morogoro vijijini.

“Tukio hilo lilitokea tarehe 08 Machi 8, watuhumiwa 11 walikamatwa wakiwa na viroba 31 vya kilogramu 50 za bangi iliyochambuliwa kwa ajili ya matumizi, misokoto 641 na miche ya bangi 26.
“Polisi waliokuwa doria katika maeneo hayo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine watano wakiwa na bangi kwenye viroba 31 vyenye ujazo wa kilogramu 50 kila kimoja,” amesema Kamanda Matei.

Imeelezwa kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakijiandaa kusafirisha mizigo hiyo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC880 BLT na T478 BWH aina ya Sanya.

error: Content is protected !!