Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wapania kupanda miti milioni 50 kufikia 2020
Habari Mchanganyiko

Wapania kupanda miti milioni 50 kufikia 2020

Miongoni mwa wanafunzi wanaoshiriki kampeni ya kupanda miti chini ya shirika la Raleigh International hapa nchini
Spread the love

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Raleigh International lenye makao makuu yake nchini Uingereza, linaendelea na kampeni yake ya utunzaji wa mazingira ukiwemo mpango wa kupanda jumla ya miti milioni 50 hapa nchini mpaka ifikapo mwaka 2020, anaandika Charles William.

Shirika hilo la kimataifa ambalo pia linajihusisha na misaada ya kijamii ikiwemo utaoji wa elimu ya ujasiriamali, lilianza kampeni ya kupanda miti milioni 50 mwezi Desemba mwaka 2016 na mpaka sasa tayari jumla ya miti 12,500 imepandwa.

“Kampeni yetu inaendeshwa kwa upandaji miti na utoaji elimu ya mazingira kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, idara za serikali zikiwemo TAMISEMI na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kampeni hii inendeshwa chini ya usimamizi wa vijana wanaojitolea.

Mwanafunzi akiwa amebeba mche wa mti tayari kwa kupandwa

“Tunahamasisha kupitia mitandao ya kijamii na mkongamano, tunashirikiana na shule za msingi, sekondari na serikali kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa. Tumefanya hivyo mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kagera, Geita, Kilimanjaro, Arusha na Manyara,” amesema Kennedy Mmmary, Ofisa Mawasiliano wa shirika hilo.

Kampeni imekuja katika kipindi ambacho takwimu za kiserikali zinaonesha kuwa, kasi ya uvunaji misitu hapa nchini kwa miaka 10 iliyopita ni kubwa kulinganisha na kasi ya upandaji wa miti, hali inayohatarisha mazingira.

Wanafunzi wakiendeleza kampeni ya kupanda miti

Takwimu hizo zinaonesha kuwa jumla ya hekta 300,000 hadi 400,000 huvunwa kila mwaka na hivyo taifa kuwa hatarini kupoteza eneo la misitu lenye ukubwa sawa na nchi nzima ya Rwanda.

Kampeni ya upandaji wa miti milioni 50 ifikapo mwaka 2020 nchini, iliyoanzishwa na kusimamiwa na shirika la Raleigh International ambalo kwa hapa Tanzania lina makao yake mkoani Morogoro pia kwa sasa inafadhiliwa na shirika la Oak Foundation.

“Kampeni hii inashirikisha jamii na kila Mtanzania mpenda mazingira. Inakadiriwa kuwa Tanzania ina jumla ya watu milioni 50 hivyo lengo la kupanda miti milioni 50 likifanikiwa ndani ya miaka mitatu ijayo, kila Mtanzania atakuwa na mti wake.

“Ni wazi kuwa tutapunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi,” amesema Mmari.

Ameishauri serikali ya Tanzania kuwasaidia vijana kuanzisha vitalu vikubwa vya miti nchini kote katika kila wilaya na miti hiyo itolewe kwa bei nafuu au bure ili jamii iweze kutambua na kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa hamasa ya upandaji wa miti milioni 50 haiwezi kufanikiwa chini ya usimamizi wa taasisi moja au kikundi cha vijana wachache bali kwa kuungwa mkono na serikali katika ngazi zote, taasisi na sekta binafsi pamoja na wadau wote wa maendeleo.

Kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika uendeshaji na utekelezahji wa kampeni hiyo, Mmari amesema kuwa changmoto kubwa ni uelewa mdogo wa dhana ya utunzaji mazingira.

“Kiukweli kuna sehemu nyingi hapa nchini ambazo jamii inategemea ukataji miti ili kuendesha maisha yao ya kila siku. Ni vigumu kwa jamii hizo kuelewa unapotoa elimu kuhusu umuhimu wa kutokata miti.

“Pia bado baadhi ya taasisi, sekta binafsi na idara za serikali hazijaipokea vyema kampeni hii, na fedha za kutosha kuendesha kampeni hii ikiwemo kununua vifaa vya kuhifadhia miti pamoja na kununua miti ni changamoto,” ameeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!