Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu ahoji Dk. Shein, Maalim kutoshtakiwa kwa uchochezi
Habari za SiasaTangulizi

Lissu ahoji Dk. Shein, Maalim kutoshtakiwa kwa uchochezi

Wakili Peter KIbatala (kushoto) akijadili jambo na mteja wake, Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), amehoji sababu za kutoshtakiwa Maalim Seif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF, Rais Ali Mohamed Shein na Hassan Nassor Moyo waliotajwa kwenye makala inayodaiwa ya uchochezi, anaandika Mwandishi Wetu.

Lissu amemuuliza swali hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani aliyekuwa akitoa ushahidi katika kesi ya tuhuma za uchochezi mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu, katika Mahakama ya Kisutu.

Kamanda Hamdani aliyekuwa akiongozwa kutoa ushahidi na Paul Kadushi, wakili wa serikali, alikumbana na swali hilo ulipofika wakati wa maswali ya kuhoji kutoka upande wa utetezi.

Katika kesi hiyo ya uchochezi washtakiwa wengine ni, Jabir Idrissa mwandishi mwandamizi wa gazeti la MAWIO na Simon Mkina mhariri wa gazeti hilo ambao kwa pamoja wanadaiwa kuandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi yenye kichwa cha habari kisemacho, “Machafuko yaja Zanzibar”.

Akijibu swali hilo la Lissu, Kamanda Hamdani amesema yeye hana jukumu la kuwafungulia mashtaka Rais Shein, Maalim Seif na Moyo hawajashtakiwa katika shauri hilo na kwamba yeye hana jukumu la kuwafungulia mashtaka.

Lissu alimuonyesha shahidi huyo gazeti la MAWIO la tarehe 14 Januari, 2016 na kumtaka amueleze Hakimu Simba idadi ya aya za makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari cha ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

“Mimi nimezisoma aya zote 55 aya 37 ni za maneno ya Maalim Seif, aya nane ni za maneno ya Tundu Lissu, aya nne ni za maneno ya Moyo na aya ya tatu, ametajwa Dk. Shein, Rais wa Zanzibar.

Lissu: Kwa uelewa wa akili yako anayetajwa mara nyingi kwenye makala hiyo inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ni nani?

Kamanda Hamdani: Maalim Seif.

Lissu: Wakati unaisoma makala hiyo ulibaini kuwapo kwa matamshi ya chuki na uchochezi dhidi ya Serikali ni kweli ama si kweli?

Kamanda Hamdani: Ni kweli.

Lissu: Kwa uelewa wako mtu anayetoa matamshi yenye kuibua hamasa au chuki dhidi ya Serikali ni lazima awe mchochezi?

Kamanda Hamdani: Ndiyo ni lazima awe mchochezi.

Lissu: (Anamuonesha shahidi huyo hati ya mashtaka na ya maelezo ya awali (PH) na kumuuliza) Ni sawa nikisema makala nzima ya ‘Machafuko yaja Zanzibar’ ilikuwa ni makala ya uchochezi?

Kamanda Hamdani: Ni sahihi.

Lissu: Kama makala yote ni ya kichochezi wote walioshiriki ni wachochezi?

Kamanda Hamdani: Ndiyo.

Lissu: Kama ndivyo, kwa nini Maalim Seif, Dk. Shein na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo hawajashtakiwa. Kwa nini Tundu Lissu pekee ameshtakiwa?

Kamanda Hamdani: Jukumu hilo siyo la kwangu, mimi ni mlalamikaji.

Lissu: Kwenye lengo lako, mbaya wako alikuwa ni Tundu Lissu?

Kamanda Hamdani: Hapana sina ubaya na Lissu.

Hakimu Thomas Simba ameiahirisha kesi hiyo hdi tarehe 03 Aprili, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

error: Content is protected !!