Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo Chadema alia na kodi
Habari za Siasa

Kigogo Chadema alia na kodi

Mashine ya kieletroniki ya kukusanya kodi
Spread the love

ONGEZEKO la kodi limetajwa kuchochea hali ngumu ya maisha inayolalamikiwa na wananchi wengi hapa nchini, anaandika Pendo Omary.

Casimir Mabina, Mratibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online kwamba mzunguko wa fedha umepotea kutokana na makali ya kodi.

“Ongezeko la kodi limeathiri mambo mengi, kwa mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya tano makali ya kodi yameongezeka na ajira zilizokuwa zikisubiriwa na watu wengi zimepeperuka ndiyo maana mzunguko wa fedha umepotea,” amesema na kuongeza;

“Bandari yetu imekosa mizigo. Tafsiri yake ni kwamba dereva wa lori la mizigo inayoenda mikoani na nje ya nchi amekosa kazi pia mama lishe aliyekuwa akimpikia dereva chakula naye hana kibarua kwa sasa.”

Mabina amesema hakuna siri kuwa hali ya sasa ya maisha ya wananchi wengi ni ngumu na uwezo wa kujipatia mahitaji yao ya kila siku umepungua kwani sukari, unga na bidhaa nyingine muhimu zimepanda bei ilihali kipato cha wananchi hakijaongezeka.

Amesema serikali inapaswa kurekebisha mfumo wa kodi ili kuwezesha uwepo kwa mfumo wa kodi utakaokaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuzalisha ajira kwa Watanzania wengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!