Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 515 wahama Ngorongoro kwenda Msomera
Habari Mchanganyiko

515 wahama Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the love

Kundi lenye kaya 72 za wananchi 515 na mifugo 2,206 limeagwa leo Alhamisi baada ya kujiandikisha na kuamua kuhama kwa hiyari kutoka katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo, Meneja wa mradi wa kuhamisha wananchi waishio ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Fedes Mdala ameeleza kuwa baada ya kundi hilo kuhama, inafikisha jumla ya kaya 749 zenye watu 4,337 na mifugo 19,915 ambayo tayari zimehama ndani ya hifadhi kwenda maeneo yaliyopangwa na serikali pamoja na maeneo mengine ambayo wananchi wamechagua.

Kamishna wa Uhifadhi NCAA, Richard Kiiza ameeleza kuwa kundi la awamu hii ndio kubwa zaidi kuondoka tangu kuanza utekelezaji wa zoezi hilo.

Aliongeza kuwa kadri ujenzi wa nyumba za makazi unavyoendelea kijiji cha Msomera, kitwai na Saunyi idadi ya wananchi wanaojiandikisha kuhama kwa hiari imeendelea kuongezeka ambapo hadi sasa zaidi ya kaya 1,070 zimeshajiandikisha kuhama na zoezi la uhamasishaji na uelimishaji linaendelea.

Kamishna Kiiza ameongeza kuwa zoezi la ujenzi wa Nyumba 5,000 katika Kijiji cha Msomera, Saunyi na Kitwai linaendeela chini ya SUMA JKT na tayari zaidi ya nyumba 360 zimeshakamilika na nyumba zingine zaidi ya 2,000 na nyumba nyingine ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kiiza amewahimiza wananchi walioagwa leo kuendelea kuwa mabalozi wa kuwahimiza wananchi waliobaki kujiandikisha kuhama kwa hiari ili wanufaike na Maisha bora yaliyoandaliwa na Serikali nje ya Hifadhi.

Akiwaaga wananchi hao Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Kanali Wilson Sakulo ameeleza kuwa wananchi wanaohama kwa hiyari wanapewa stahiki zao zote za msingi ikiwepo nyumba yenye hati kwenye eneo la ukubwa wa ekari 2.5, shamba la kulima la ekari tano, huduma za maji, shule, afya, barabara, mabwawa, majosho, minada, umeme na huduma za mawasiliano na kupata uhuru wa kufanya shughuli za kilimo na kuishi Maisha huru tofauti na hifadhini.

Kanali Sakulo ameelekeza uongozi wa NCAA kuendelea kutoa elimu, uhamasishaji na uandikishaji kwa wananchi walio tayari kuhama kwa hiari na kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliyejiandikisha kuhama anahamishwa kwa wakati, kupata stahiki zake zote.

Pia amesema anahakikisha wananchi wanaohama hawarudi tena maeneo ambayo wameshahama kwa kuwa Serikali yetu imeshawajengea mazingira wezeshi yenye huduma zote muhimu za kijamii.

Mmoja ya wananchi aliyehama Petro Tengesi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwa wananchi wa Ngorongoro na kuendelea kuwajengea mazingira bora nje ya hifadhi ikiwemo ulipwaji wa stahiki zao za kuhama, kusafirishiwa mizigo yao pamoja naa kuboreshewa huduma za kijamii nje ya hifadhi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!