Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 25 wafariki dunia katika ajali Arusha
Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the love

Watu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo, kati ya watu hao watatu ni wa familia moja ya Abdulrazak Mohamed maarufu ‘Chucha’ wa Ngaramtoni.

Akizungumzia na waandishi wa habari Kamanda Masejo amesema ajali hiyo imetokea leo tarene 24 Februari majira ya saa 11 jioni baada ya lori lililokuwa likitokea Namanga kuelekea Arusha kuyagonga magari matatu.

Bila kutaja jina la dereva aliyekuwa akiendesha lori hilo, Kamanda Masejo amesema taarifa za awali zinaonyesha Lori  lilipoteza uelekeo hali iliyopelekea kuyagonga magari hayo.

Amesema majeruhi wa ajali hiyo wapo katika hali mbaya na wanaendelea na matibabu.

 Hata hivyo, amewaomba wananchi ambao ndugu zao walikuwa wakisafiri kupitia barabara hiyo kufika katika hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kwa ajili ya utambuzi wa marehemu pamoja na majeruhi ambao wanatibiwa hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!