April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watakaoandamana tutawashughulikia – Polisi

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa onyo kwa watu wanaopanga kufanya maandamano kesho tarehe 7 Julai 2020, kwa ajili ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020 na SACP Lazaro Mambosasa, kamanda wa kanda hiyo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Amesema, watu watakaofanya maandamano hayo aliyoita kuwa ni batili, watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Jeshi linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 7 Julai 2020, kwa madai ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi, waache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Kamanda Mambosasa.

Wazo la kufanyika maandamano kwa ajili ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi liliibuliwa hivi karibuni Dk. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera.

Wazo hilo liliungwa mkono na baadhi ya watu, hasa watumiaji wa mtandao wa Twitter, ambapo wameanzisha kampeni ya ‘77  nyeupe’ kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wenye nia ya kudai tume hiyo, kuvaa nguo nyeupe siku hiyo, kama ishara ya kudai haki hiyo.

error: Content is protected !!