Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Viongozi wadini wapewa kazi kudhibiti Ebola
AfyaTangulizi

Viongozi wadini wapewa kazi kudhibiti Ebola

Spread the love

VIONGOZI wa dini zote wametakiwa kushirikishwa kwenye maandalizi ya mapambano ya ugonjwa wa ebola ambao umetaatifiwa upo nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo endapo itatokea utaingia nchini Tanzania ili kuweza kuutokomeza kabisa. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati alipotembelea Mkoa wa Kigoma akiongozana na timu yake ya wataalam kwa ajili ya ukaguzi wa nyenzo na afua mbalimbali zilizowekwa ili kupambana na ugonjwa wa ebola leo Mkoani humo.

“Afua muhimu ya mkoa wowote katika kupambana na ugonjwa huu ni kuwashirikisha vizuri viongozi wa dini zetu pamoja na viongozi wa kimila na jamii kwani ndio wanaokutana na wanajamii kwa muda mwingi zaidi hivyo kuwashirikisha kwao elimu juu ya kujikinga na Ebola itakuwa kubwa zaidi na hatimae tutafanikiwa kujikinga na ugonjwa huu,” amesema Prof. Bakari.

Aidha Prof. Bakari Kambi amesema kuwa Mkoa wa Kigoma upo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa Ebola kwa kuwa kuna mipaka mingi iliyo wazi ambayo inaingiza wageni kutoka Burundi na Congo ambapo ugonjwa huo umetaarifa upo maeneo ya nchi ya Congo.

Mbali na hayo Prof. Bakari Kambi ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa jitihada na mikakati waliyoiweka na kuifanyia kazi ili kuweza kudhibiti ugonjwa wa Ebola endapo utaingia Mkoani humo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Paul Chaote amesema hadi sasa Kigoma hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika maeneo yote ya mkoa huo.

“Utambuzi wa joto la Mwili kwa wageni kutoka nchi jirani ya Congo wanaoingia kupitia bandari ya Kigoma, Manyovu, Kibirizi, Mabamba, Uwanja wa Ndege, Kituo cha Gari Moshi bado unaendea kufanyika kwa uhakika kwa kutumia Thermo scanner ili kudhibiti ugonjwa huo,” amesema Dk. Chaote.

Aidha Dk. Chaote amesema bado wanaendelea kutoa elimu kwa jamii, watumishi wa Afya, madereva wa magari ya kubebea wagonjwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kujikinga na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.

“Tumetoa mafunzo kwa timu za kitaalam mbalimbali za mkoa pamoja na kuhakikisha madawa, vifaa tiba na PPE vipo vya kutosha wakati wote katika vituo vyote vilivyoanishwa kupokea na kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola,” amesema Dk. Chaote.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi ameambatana na jopo la wataalam ikiwemo idara ya uhakiki ubora wa huduma za afya, Kitengo cha Dharura na Maafa, Elimu ya Afya kwa Umma, Kitengo Cha mawasiliano Wizara ya Afya zote kutoka Wizara ya Afya pamoja na wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kukagua na kujiridhisha mikakati ya kujikinga na Ebola endapo itaingia nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

Habari za SiasaTangulizi

CDF Mabeyo: Magufuli alijua anakufa

Spread the love  ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Venance Mabeyo,...

AfyaBiashara

Meridianbet yatoa msaada zahanati ya Mwenge

Spread the love MABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet wamefanikiwa kufika eneo...

AfyaTangulizi

Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF

Spread the loveSERIKALI imesema imeondoa dawa 178 katika kitita cha Mfuko wa...

error: Content is protected !!