Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Kamati ya waamuzi yasimamisha watano
Michezo

Kamati ya waamuzi yasimamisha watano

Spread the love

KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mzee Salum Chama imewasimamisha baadhi ya waamuzi ambao wamefanya vibaya kwenye michezo ya raundi ya kwanza na ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Waamuzi waliosimamishwa kupisha uchunguzi ni pamoja na mwamuzi msaidizi namba 2 (Line 2) Godfrey Msakila kutoka Geita mchezo kati ya Yanga dhidi Mtibwa Sugar, Msakila ambaye anadaiwa kukataa goli la Makambo kwa kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea.

Mwamuzi mwingine ni Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro (Line 2) mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa naye amesimamishwa kwa kulalamikiwa kuzuia shambulizi la Mtibwa akidai Ismail Aidan alikuwa ameotea huku picha za video za marudio ya tukio hilo zikionyesha hakuotea.

Wengine ni Nassoro Mwinchui na msaidizi wake Abdallah Rashid wa Pwani wamesimamishwa kwa kosa la kukataa goli la Biashara United katika mechi ya Coastal Union dhidi ya Biashara wakidai mfungaji alikuwa ameotea.

Pia, Mwamuzi msaidizi Nicholas Makaranga wa Morogoro amesimamishwa kwa kukataa goli la Ruvu Shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji Fully Zullu Maganga alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.

Adhabu hiyo pia haijamuacha mwamuzi msaidizi Ahmada Jamada kutoka Kagera ambaye alikataa goli la kusawazisha la Mwadui FC dhidi ya Singida United juzi Jumapili kwa madai ya kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Aidha, Mwenyekiti wa hiyo amesema kuwa waamuzi hao walichezesha chini ya kiwango na kupata alama chache zilizopelekea kusimamishwa kwao ili kupisha uchunguzi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!