Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi EALA vurugu tupu
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi EALA vurugu tupu

Ezekia Wenje, aliyekuwa mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

SEHEMU kubwa ya umma wa Watanzania imeshtushwa mno na namna uchaguzi mkuu wa wajumbe wa kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki ulivyoendeshwa, anaandika Jabir Idrissa.

Chumba cha habari cha kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) kilianza kupokea simu za wananchi wakitoa maoni ambayo mengi yameashiria kutoridhishwa na uendeshaji wa uchaguzi huo.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana jioni lilifanya uchaguzi wa wajumbe wa bunge la Afrika Mashariki ndani ya kinachostahili kuelezwa kuwa ni “vurugu tupu.”

Vurugu zilitawala uchaguzi huo huku kambi ya upinzani ikijikuta inaamuliwa kila kitu hata pale hoja zake zilipokuwa zinalielekeza bunge katika umuhimu wa kuzIngatia sheria na kanuni za kuendeaha uchaguzi huo.

Dunstan Faustine akilalamikia alichokiita “uchagzui wa aibu kubwa” alisema hajapata kuona uvurugaji wa taratibu za uchaguzi ndani ya bunge kama alivyoshuhudia jana.

“Kila ninavyojiuliza sipati jibu kwamba tulikuwa na haja kweli ya kupata wabunge kwa njia ile ya ukiukaji kanuni za bunge.”

“Sidhani kama Taifa letu linastahili kuonekana la watu wasioheshimu sheria namna ile tena wale viongozi wanaotarajiwa kuongoza njia wakawa waongoza ujinga,” alisema Dunstan aliyepiga simu usiku jana.

Baraka Shamsi anayeishi Upanga jijini Dar es Salaam alipiga simu asubuhi leo na kusema kwa aliyoyaona anaogopa hata kujitambulisha kama ni Mtanzania.

Anasema kwa shughuli zake za kusafiri kama mfanyabiashara anahofia kuchekwa na washirika wake nchini Kenya.

“Nitajitetea vipi katika uchaguzi uliojaa vurugu kutokana na kuvunjwa makusudi sheria na kanuni zake…

“Nilivoona CCM ingetaka basi wabunge wote tisa wangetoa wao. Hawakutaka kabisa upinzani upate haki yake ya kutoa wawakilishi.”

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema uongozi wa bunge uliongoza uvurugaji wa taratibu kwa maelekezo ya wakubwa wa Chama Cha Mapinduzi.

Katika andishi lake la leo amesema kwa mfano, Katibu wa Bunge alijifanya mwamuzi lakini kwa hakika “alikuwa kocha wa CCM.”

Hapa chini alichoandika Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu baada ya uchaguzi huo.

Wakubwa habari za asubuhi.

I’m still licking my wounds, kama wasemavyo Waingereza.

Pamoja na kwamba vumbi la uchaguzi wa jana bado limetanda, naomba niseme yafuatayo juu ya uzoefu wa hizi siku chache zilizopita.

1) Kuna wanaodai tulikosea kutokuangalia gender balance ndio maana tumeshindwa.

Hapana.

Kosa letu sio kutokuzingatia jinsia. Kosa letu kubwa na lisilosameheka ni kuwa chama kikuu cha upinzani dhidi ya MaCCM. Na tumelifanya kosa hilo tangu mwaka 2010.

Wenzetu wa CUF nao walishawahi kufanya kosa hili kubwa miaka ya nyuma na mnakumbuka yaliyowapata. Na NCCR Mageuzi kabla ya CUF.

2) Kosa letu la pili ni kuwa chama kikuu cha upinzani lakini bila kuwa na nguvu ya kutosha bungeni kuzuia njama za MaCCM ndani na nje ya Bunge.

Ni hivi. Sisi wa UKAWA tupo 116, MaCCM yako 252 na bado wanajiongeza i.e. Salma Kikwete na wengineo watokao Magogoni. Wao wana 70%, sisi tuna 30% ukihesabu kila mtu aliyeko bungeni.

Kwa balance hii hata tukifanyaje tutaonewa tu. Na chochote tutakachopata itakuwa ni kwa fadhila yao.

Kwa sababu ya balance hii, hawahitaji hata kuheshimu sheria na kanuni za Bunge.

Kati ya Jumamosi na jana wamebadilisha sheria na kanuni za uchaguzi kwa namna ambayo inatisha.

In fact, hawakufuata chochote kilichoandikwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Badala yake, walibadilisha kanuni kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea na kadri ya mahitaji ya maslahi yao.

Kanuni inavipa vyama vya siasa haki ya kuweka mgombea mmoja hadi watatu kwa kila nafasi inayogombaniwa. Ndivyo tulivyofanya. Machoni pao tulikosea sana.

Kwa practice ya Bunge letu, wagombea wasiokuwa na mpinzani hupita bila kupingwa. Na hii ndio sheria yetu ya uchaguzi hata nje ya Bunge. Jana imebadilishwa.

Wagombea wa CUF walikuwa wanne kwenye nafasi moja wakati kanuni zinasema maximum ni wagombea watatu kwa nafasi moja.

Watatu kati ya hao hawakuwa na fomu za uteuzi zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF kama ilivyotakiwa na kanuni. Bali, kwa kauli ya Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi, majina yao yalitokea NEC.

NEC inahusikaje na uteuzi wa majina ndani ya vyama, mimi sijaelewa bado.

Kura zilipigwa kwa utaratibu usiokuwepo kwenye kanuni kabisa. Hakuna upigaji wa kura ya ndio au hapana kwenye uchaguzi wa EALA. Lakini wamepigia wagombea wetu au hapana.

Hakuna utaratibu wa wengine wanapigiwa kura ya ndiyo tu lakini wengine wanapigiwa ndio au hapana kwenye karatasi hiyo hiyo moja ya kura. Jana wagombea saba wamepigiwa kura za ndio tu, wawili wamepigiwa ndio au hapana.

Kanuni inasema usipochagua wagombea tisa basi kura yako imeharibika. Jana wamepigia kura wagombea saba tu na hakuna kura yoyote iliyoharibika.

Kanuni inaelekeza kura kuwa ya siri lakini jana usiku hakukuwa na kura yoyote ya siri.

Na mengine mengi.

Yote haya yanatokana na dominance ya MaCCM bungeni. Na juu ya yote haya, ongezea la Msimamizi wa Uchaguzi ambaye anajifanya ni refa wa mchezo huu lakini kiuhalisia ni kocha wa timu ya MaCCM.

Katika mazingira haya, je, watu hawa wataitisha uchaguzi mwingine ili kujaza nafasi mbili za CHADEMA zilizobaki???

Hili ni kwa wale wanaofikiria tukiongeza jina moja au mawili basi shida itakwisha na MaCCM yatatupatia nafasi zetu. Mimi sina jibu lake lakini hisia zangu zinaniambia hii imetoka.

Nitaendelea wakati mwingine.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!