Donald Trump, Rais wa Marekani

Trump, Melania watinga Iraq kimyakimya

Spread the love

ZIARA ya Rais wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania imefanywa kimyakimya nchini Iraq. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea).

Hata hivyo inaelezwa kuwa, utawala wa Iraq ulikuwa na taarifa ya ujio huo na kuwa, Waziri Mkuu wa Iraq alipanga kukutana naye.

Hata hivyo Trump ameondoka Iraq bila kukutana na mwenyeji wake waziri mkuu Adel Abdul Mahdi kwa madai kuwa, kushindwa kukubaliana jinsi mkutano huo ungefanyika.

Trump na mkewe walisafiri usiku wa Krismasi kwenda nchini humo kuzungumza na wanajeshi wake ambapo aliwaambia Marekani haina mpango ya kuwaondoa kwenye ardhi ya Iraq.

Trump aliwashukuru wanajeshi wake nchini humo kwa kujitolea. Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo.

Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Iraq kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi la Islamic State.

ZIARA ya Rais wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania imefanywa kimyakimya nchini Iraq. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea). Hata hivyo inaelezwa kuwa, utawala wa Iraq ulikuwa na taarifa ya ujio huo na kuwa, Waziri Mkuu wa Iraq alipanga kukutana naye. Hata hivyo Trump ameondoka Iraq bila kukutana na mwenyeji wake waziri mkuu Adel Abdul Mahdi kwa madai kuwa, kushindwa kukubaliana jinsi mkutano huo ungefanyika. Trump na mkewe walisafiri usiku wa Krismasi kwenda nchini humo kuzungumza na wanajeshi wake ambapo aliwaambia Marekani haina mpango ya kuwaondoa kwenye ardhi ya Iraq. Trump aliwashukuru wanajeshi wake nchini humo kwa kujitolea. Ziara…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!