Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wakulima Dodoma wapewa somo
Habari Mchanganyiko

Wakulima Dodoma wapewa somo

mazao la Alizeti
Spread the love

WAKULIMA wa Mkoa wa Dodoma wametakiwa kulima mazao ambayo yanaendana na hali ya hewa ili kuweza kupata mazao mengi. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa na Afisa kilimo Mkoa wa Dodoma, Brnard Abraham alipokuwa akizungumaza na waandishi juu ya uhamasishaji wa kilimo chenye tija kwa wakulima wa Mkoa wa Dodoma.

Mbali na kuwataka wakulima kulima mazao ambayo yanaendana na hali hewa pia amewataka wataalamu wote wa kilimo kuwa karibu na wakulima kwa maana ya kuhamishia ofisini mashambani kwa lengo la kuwasaidia wakulima ndani ya Mkoa huu.

Abraham alisema kuwa yapo malalamiko kuwa wataalamu wa kilimo ni wachache katika maeneo ya mashamba jambo ambalo alisema kuwa kwa Tanzania hakuna sekta yoyote ambayo imejitoshereza lakini watumishi au wataalamu wamekuwa karibu na wadau wao.

“Kipindi hiki ni kipindi cha maadalizi ya mashamba hivyo nawashauri wakulima kulima kilimo ambacho kinaendana na mazingira husika kutokana na hali ya hewa, wapo wakulima ambao wanalazimisha kulima mazao ambayo hayaendani na hali ya hewa husika.

“Ni lazima kulima kilimo chenye tija na kinachoweza kumuinua mkulima kimaisha na taifa kwa ujumla wake lakini kama wataendelea kulima kilimo ambacho ni cha mazoea ni wazi kuwa wataendelea kulima kilimo cha kujikimu badala ya kuwa na kilimo chenye tija.

“Hata hivyo nawaagiza wataalamu wa kilimo kuwa karibu na wakulima kwa maana ya kuwaelekeza ni jinsi gani ya kuwashauri wakulima ili walime kilimo cha kisasa na chenye tija badala ya kulima maeneo makubwa lakini hayana tija na mazao wanayovuna ni kiduchu,” alisema Abraham.

Katika hatua nyingine Abraham alisema pia wakulima wana wajibu wa kuwa karibu na wataalamu wa kilimo pale wanapokuwa wakihitaji ushauri au maelekezo au pale wanapoona kuwepo kwa dalili wazizozielewa ili waweze kupatiwa ushauri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!