Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Serikali, maaskofu wavurugana Zimbabwe
Kimataifa

Serikali, maaskofu wavurugana Zimbabwe

Spread the love

NCHINI Zimbabwe, Serikali imegoma kupokea barua iliyoandikwa na Baraza la Maaskofu la Katoliki ikilalamikia vitendo vya rushwa, unyanyasaji, umasikini na haki za binadamu. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kwenye barua hiyo, maaskofu hao wameeleza namna Taifa hilo likishindwa kukabiliwa na changamoto za kuchumi na kisiasa huku likiagiza kufanyika uamuzi wa haraka kujinusuru.

Hata hivyo, katika hali ya mshangao, Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa imegoma kupokea barua hiyo huku ikisisitiza “hakuna janga la kisiasa wala kiuchumi.”

Nick Mangwana, Katibu wa Habari nchini humo ameshusha lawama zake kwa maaskofu hao, kwamba wanaligawa Taifa kwa kuanzisha makundi hivyo kuiingiza nchi hiyo kwenye machafuko.

Wananchi wa Zimbabwe wamekuwa kwenye maandamano wakiishutumu serikali kushindwa kukabiliana na kudorora kwa uchumi pamoja na kutamalaki kwa rushwa.

Barua ya maaskofu inaeleza kuwa, hali mbaya iliyopo kwa sasa Zimbabwe, imesababisha uchumi kuanguka, kuongezeka kwa umasikini na ukiukaji wa haki za binadamu.

Baraza hilo limetia mkazo kwamba, rushwa ndani ya serikali ya Rais Mnangagwa imekithiri na kuwa katika kiwango cha hatari “rushwa imefikia kiwango cha hatari mno.”

Hata hivyo, Rais Mnangagwa anaelekeza tuhuma zake kwa wapinzani wake kwamba wanashirikiana na wageni kuangamiza taifa hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!