Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Msikiti wa Mtoro Dar uliofungwa, wafunguliwa
Habari Mchanganyiko

Msikiti wa Mtoro Dar uliofungwa, wafunguliwa

Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika ibada katika Msikiti wa Mtoro, Kariakoo
Spread the love

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limeamua kuufungua Msikiti wa Mtoro, ulioko maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, uliopangwa kufungwa kwa muda wa wiki mbili, kufuatia taharuki ya janga la Virusi vya Corona. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu tarehe 4 Mei 2020, Alhad Mussa Salum, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema msikiti huo utafunguliwa rasmi Jumatano ya tarehe 6 Mei 2020.

Amesema Baraza la Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, limeamua kuufungua msikiti huo pamoja na misikiti mingine iliyofungwa mkoani humo, ili kuwapa nafasi waumini wa dini ya Kiislamu, kufanya ibada katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani unaoendelea.

“Juzi tulitoa tamko la kuufunga Msikiti wa Mtoro kwa sababu tulizozieleza. Baraza kwa kushirikiana na uongozi wetu wa juu, ilionekana ni vyema zichukuliwe hatua kutokana na yaliyotokea na tukatamka kufunga msikiti wa Mtoro kwa wiki mbili,” amesema Sheikh Alhad.

“Lakini mimi na baraza langu la masheikh tumekwenda kufungua misikiti hiyo kwa sababu ni mapenzi yetu kama BAKWATA kuona Waislamu wanafanya ibada Mwezi wa Ramadhani,” amesema.

Alhad Mussa amesema wataalamu wa wizara ya afya kesho Jumanne wataonana na uongozi wa Msikiti wa Mtoro, kwa ajili ya kutoa maelekezo juu ya taratibu za kiusalama wakati ibada zikiendeshwa msikitini hapo.

“Kwa hiyo misikiti haikufungwa na haitafungwa lakini ilitokea Mtoro kufungwa kwa sababu. Kwa kutafakari zaidi tumeona Msikiti wa Mtoro ufunguliwe, kwa maana zile dharura ambazo zingetufanya tutumie wiki mbili zitaondolewa,” amesema Alhad Mussa

Sheikh huyo wa mkoa amesema, “Baada ya kushauriana Msikiti wa Mtoro tutaufungua siku ya kesho kutwa (Jumatano), kesho tutatembelewa na wataalamu wa wizara ya afya, watazungumza nasi kupeana namna ya kufuata taratibu za kiusalama juu ya hatari ya Virusi vya Corona. Siku ya Jumatano alfajiri msikiti wetu utafunguliwa.”

Msikiti huo ulifungwa tarehe 2 Mei 2020 baada ya video inayoonyesha mkusanyiko wa watu waliokwenda kuswali Swala ya Ijumaa msikitini hapo, kusambaa mitandaoni, hali iliyotafsiriwa kwamba ingesababisha kusambaa kwa virusi vya corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!