April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

SAKATA LA MEYA UBUNGO: Tamisemi yaingilia kati 

Spread the love

HATMA ya Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, sasa iko mikononi mwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

“Tayari mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Betrice Dominic, tayari amemaliza wajibu wake. Hawezi kubadilisha maamuzi ya kile alichokitenda.  Ninachosikitika ni kwamba mpaka sasa, hatuna barua ya Jacob badala yake tunasikia matamko kutoka kwa John Mnyika,” ameeleza Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mwita Waitara.

Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma, leo Jumatatu, Waitara alisema, tayari TAMISEMI ilishapokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, kutujulisha kuuhusu kuondolewa kwa meya huyo.

Waitara amesema, “mjadala wowote kuhusu nafasi ya meya wa ubungo haipaswi kuwa katika mazungumzo tena kwani Tamisemi inatambua hakuna meya Ubungo.”

Ameingeza: “Katibu mkuu wa Chadema hana mamlaka hata kidogo ya kumtaka mkurugenzi kufanya jambo lolote hivyo kutoa tamko kuhusu mkurugenzi ni kujichanganya.”

Akijibu swali ikiwa Chadema ambako yeye alihudumu hadi nafasi ya ubunge, kama katiba yake inaruhusu kata kumfukuza diwani, Waitara amesema, katiba ya chama inaruhusu hata tawi kumfukuza diwani kama anakwenda kinyume na maadili na matakwa ya chama.

Alisema Katiba ya Chadema iko wazi namna anavyoifahamu na kama haijabadirika bado iko sahihi na walioandika barua wako sahihi hakuna walipogushi.

Amemtaka Boni badala ya kuhangaika kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kutafuta huruma, Waitara amesema, “ni vema akaleta rufaa kwetu au aende mahakamani.”

Jacob alitangazwa kutokuwa meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Ubungo, juzi Jumamosi, kufuatia uongozi wa kata yake ya ubungo, kumuandikia barua mkurugenzi wa manispaa hiyo, kuwa amevuliwa uwanachama.

error: Content is protected !!