July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji ya diwani mteule CCM, tisa washikiliwa                             

Spread the love

WATU tisa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya Fatuma Ngozi, aliyekuwa diwani mteule wa Kata ya Kikongo, Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani…(endelea).

Mbali na mauaji ya Fatuma yaliyotokana na kuchomewa nyumba yake akiwa ndani, watu wengine watatu walifariki dunia kwenye tukio hilo lililotokea tarehe 9 Novemba 2020.

Kwa mujibu wa Wankyo Nyigesa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, tukio hilo lilitokea saa saba usiku katika Kijiji cha Chekeleni, Kata ya Kikongo , Tarafa ya Mlandizi kwenye Halmashauri ya Kibaha Vijijini.

Kwamba, mbali na watu wawili waliokuwa kwenye nyumba hiyo wakati wa tukio kufarika, we ngine watatu walifariki wakati wakipatiwa matibabu na kufanya jumla ya watu waliofariki kuwa sita huku mmoja aliendelea na matibabu.

Wankyo Nyigesa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,

Kamanda Nyigesa amesema, baada ya uchunguzi wa jeshi lake, limekamata watu tisa ambapo wanane ni wanaume na mmoja ni wanawake, akifafanua zaidi amesema ‘watu hao wamekamatwa kutokana na ushahidi uliokuswanywa.”

Amesema, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewahoji watuhumiwa wote, na sasa taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

Fatuma Ngozi, aliyekuwa diwani mteule wa Kata ya Kikongo, Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) enzi za uhai wake

“Uchunguzi wa tukio bado unaendelea, jeshi la polisi litaendelea kuhifadhi majin a, kazi na wadhifa wa watuhumiwa hawa. Kadhi tutakavyokuwa tunaendelea kupeleleza, tutakamata wengine kwa mujibu wa upelelezi wetu,” amesema.

error: Content is protected !!