Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Abel & Fernandes, St. Laurent wajitosa kudhibiti kisukari
Habari Mchanganyiko

Abel & Fernandes, St. Laurent wajitosa kudhibiti kisukari

Mkurugenzi wa Kituo cha Kisukari- St Laurent, Dk. Mary Maige
Spread the love

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara ili kudhibiti magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari ambao hadi sasa umeathiri zaidi ya watu milioni 1.5. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Abel & Fernandes, Fatma Fernandes  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Kisukari duniani yaliyofanyika Kituo kinachotoa huduma za Kisukari  St. Laurent jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 14 Novemba 2020, yalienda sambamba na utoaji wa huduma za upimaji na ushauri wa kitabibu bure.

Katika maadhimisho hayo ya mwaka 2020, yalidhaminiwa na  Kampuni ya Abel & Fernandes Communications pamoja na Quincewood Consulting kupitia miradi yake ya uwajibikaji kwa jamii.

Mkurugenzi wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes akichukua maelezo mmoja wa waliojitokeza kupima afya zao katika upimaji na ushauri wa kitabibu bure.

Aidha, katika maadhimisho hayo, kampuni hizo zimeungana na Kituo cha Kisukari St. Laurent katika kuisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya Kisukari kwa kujenga uelewa kuhusu ugonjwa huo ambao kwa mujibuwa takwimu za wizara ya afya hadi sasa umeathiri zaidi ya watu milioni 1.5 nchini.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kisukari- St Laurent, Dk. Mary Maige alisema, kauli mbiu ya maadhimisho ya Kisukari duniani  kwa mwaka huu ni “Uuguzi na Kisukari.”

Alisema mwaka 2012 walifanya utafiti nchi nzima na kubaini kati ya watu 10, watu watano wana tatizo la kuchakata sukari mwilini hivyo kubaini kuwa asilimia 20 ya Watanzania wana matatizo ya kuchakata kisukari.

“Kwa hiyo, hili tatizo linazidi kuongeza na kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, tatizo linaendelea kuongezeka na tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kudhibiti tatizo hili ambalo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wetu wa maisha,” alisema.

Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Johari Yusufu alisema kampeni hiyo ya mwaka huu inalenga kuwapa motisha wauguzi kutekeleza majukumu yao kwa uweledi ili kuwapatia huduma bora, stahiki na zenye staha wagonjwa wa kisukari nchini.

Alisema wauguzi wanahesabika kuwa nusu ya wafanyakazi wote wa sekta ya afya nchini. Ni kada mojawapo inayoweza kuwapatia huduma bora watu wanaoishi na magonjwa mbalimbali. Watu wanaoishi na Kisukari huhitaji zaidi msaada wa wauguzi katika kutibu tatizo hilo.

“Kwa hiyo tunawashauri wananchi wawe wanakwenda hospitali kucheki afya zao mara kwa mara,” alisema.

Aidha, Meneja uhusiano wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communications, Abbas Jabir alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa pamoja wanaungana na wauguzi kuzuia na kutoa muongozo kuhusu Kisukari.

“Pia tunatoa huduma kwa mamia ya jamii kwa malengo ya kuwapatia taarifa muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kukabiliana nao,” alisema.

“Maadhimisho ya mwaka huu ni muhimu kwetu wote kwani yanatoa fursa ya kupata huduma za afya bure kwa malengo ya kuboresha afya za watanzania wanaoishi na Kisukari, pia kuboresha maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa huo,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!