WAZIRI wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangala wamekutana na Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke kuongelea masuala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa wanyamapori na vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).
Waheshimiwa Mawaziri na Balozi pia wameongelea kuhusu mkutano wa utunzaji wa wanyamapori na udhibiti wa biashara ya wanyamapori ulioandaliwa na Serikali ya Uingereza na unaotarajiwa kufanyika wiki hii jijini London.
Aidha, Balozi Cooke ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwezesha ziara ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William iliyofanyika hapa nchini.
Leave a comment