October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya Dunia yampa ‘saluti’ JPM

Rais John Magufuli

Spread the love

BENKI ya Dunia (WB) imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhili hapa nchini, unaofanmywa na serikali ya Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wake na Rais Magufuli uliofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird ameeleza kuwa, maendeleo ya utekelezaji  wa  miradi inayofadhiliwa na WB hapa nchini ni mazuri.

Kufuatia kuridhishwa na maendeleo hayo, Bird  amesema WB iko katika mchakato wa mwisho wa maandalizi ya ufadhili wa miradi mingine katika sekta ya elimu, hasa elimu ya awali na sekondari itakayogharimu kiasi cha Sh. 1.357 trilioni.

Hadi sasa kuna miradi yenye thamani  ya 10.186 trilioni inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ambayo iko katika hatua ya utekelezaji.

error: Content is protected !!