November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba alalamika rafu Uchaguzi Liwale

Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, anadai kuna uwepo wa rafu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Liwale unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Oktoba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 9 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amedai kuwa, kuna njama zinazofanywa na baadhi ya watumishi wa umma kwa minajili ya kukibeba Chama cha Mapinduzi CCM katika kulitwaa jimbo la Liwale kupitia uchaguzi huo.

Prof. Lipumba ameeleza kuwa, CCM inatambua kwamba CUF ina nguvu Liwale na hivyo inataka kutumia nguvu kulichukua jimbo hilo lililowazi baada ya ya aliyekuwa mbunge wake, Zubeir Kuchauka kujiuzulu na kurudi CCM.

Kufuatia madai hayo, Prof. Lipumba ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa uchaguzi huo ikiwemo maandalizi yake kwa ajili ya kuzuia njamana ili uwe wa haki.

error: Content is protected !!