Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Cedric Kaze kocha mpya Yanga
Michezo

Cedric Kaze kocha mpya Yanga

Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Yanga umemtangaza Cedric Kaze kuwa kocha mpya wa klabu ya Yanga, ambaye atakiongoza kikosi hicho katika misimu ujao wa mashindano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Kaze ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Luc Eymael ambaye alidumu ndani ya klabu hiyo kwa miezi saba, na baadae kutimuliwa baada ya msimu wa ligi kumalizika.

Jina la kocha huyo limetajwa leo la M/kiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msolwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya Mwananchi uliofanyika mapema hii leo jijini Dodoma.

Msolwa amesema kuwa kocha huyo atafika nchini ndani ya siku za hivi karibuni huku tayari benchi lake la ufundi likiwa limeshakamilika na hawatoweza kutangaza mpaka kocha huyo afike.

“Kocha ameshapatikana, anaitwa Cedric kutoka Burundi ambaye sasa hivi anaishi Canada ambaye siku hizi mbili anakuja, huku benchi lake la ufundi limeshakamilika, na tutampa sapoti” alisema Msolwa

Aidha aliongezea kuwa kocha msaidizi ameshapatikana na Cedric ndiye aliyempendekeza kufanya nae kazi ndani ya kikosi hicho.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya yanga zinasema kuwa kocha huyo amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili mpaka 2022.

Yanga mpaka sasa imeshabadili makocha watatu katika kipindi cha mwaka mmoja, ikimbukwe klabu hiyo ilianza msimu 2019/20 chini ya kocha Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa 5 Novemba, 2019 na nafasi yake ikachukuliwa na Luc Eymael ambaye nae alidumu ndani ya kikosi hicho kwa miezi saba tu, na baadae kutimuliwa na mapema hii leo wamemtangaza kocha huyo.

Kaze ambaye ni raia wa Burundi anamiliki lesseni daraja la kwanza ya Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) pamoja na leseni ya Chama cha soka Ujerumani Deustcher Fussball Band (DFB).

Aidha kocha huyo ameshawahi kufundisha timu za Taifa za Burundi chini ya umri wa miaka 17, 20 na 23, pia ameshafanya kazi kwenye akademi ya Barcelona.

Cedric Kaze amewahi kuwafunga Yanga mabao 2-0 wakati akiifundisha Atletico Olympic walipokutana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!