Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kongamano la kitaifa kuwakutanisha viongozi Dodomna, JPM mgeni rasmi
Habari za Siasa

Kongamano la kitaifa kuwakutanisha viongozi Dodomna, JPM mgeni rasmi

Rais John Magufuli
Spread the love

JUMUIYA ya Maridhiano Tanzania inaratajia kufanya kongamano la maombi kwa ajili ya kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kongamano hilo litakalofanyika tarehe 24 Agosti 2020 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Akizungumza na vyombo vya habari jana Ijumaa tarehe 21 Augosti 2020, jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano, Sheikk Alhad Mussa Salum, alisema, lengo kubwa la kongamano hilo kuombea uchaguzi pamoja na kuwaweka pamoja viongozi wa kisiasa na kulinda amani ya nchi kwa ujumla.

”Kongamano la maombi litakuwa na mada mbalimbali ambazo zitatolewa na wachungaji, Maaskofu, Mashekh na mapadre lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaelezea masuala mbalimbali ambayo yatadumisha amani katika taifa hususani wakati wa kipindi cha uchaguzi.”

“Pamoja na mambo mengine ambayo yatakuwa ndani ya mada ni kuitaka tume ya uchaguzi kuhakikisha inatenda haki na kutoa haki kwa vyama vyote ili bila kuwa na upendeleo kwa nia ya kulinda na kutunza amani ya nchi,” alisema Salum ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Sheikk Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano

“Yapo maisha baada ya uchaguzi kwa maana hiyo, jumuiya ya maridhiano kwa kufanya kazi zake kwa kwawaunganisha viongozi wa dini pamoja na serikali ni lazima tuhakikisha tunasimamia misingi ya haki, upendo, mshikamano na amani katika nchi,” alisema

Kuhusu kongamano hilo, Sheikh Salum alisema kutokana na kuwepo kwa viashiria vinavyoonekana kujitokaza kama vile kuchomwa ofisi za baadhi ya vyama, kuwepo kwa kauli za kejeli na kashifa kwa baadhi ya wagombea wa vyama vyote vya siasa wameona umuhimu wa kufanyika kwa kongamano hilo.

”Hatuhitaji siasa za chuki nchini, tunahitaji kuwa na wagombea ambao wanatangaza sera zao na ikumbukwe katika mikutano ya siasa kuna watoto wetu hivyo hatutaki kusikia mambo ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Maridhiano Mkoa wa Dodoma, Mchungaji Evance Lukasi Chande wa Kanisa la EAGT Nazael Ipagala alisema Kongamano hilo linalenga kuwajenga Watanzania wote kuendelea kuwa wamoja katika shughuli zao za kila siku.

Alisema siyo mataifa yote ambayo yanatamani kuona taifa la Tanzania na Watanzania kwa ujumla wakiendelea kuwa na amani, upendo na mshikanano.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano mkoa wa Dodoma kwa upande wa akina mama, Pili Yomba aliwasisitiza akina mama kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika kongamano hilo kwa lengo la kujifunza mambo mengi na ya muhimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!