CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, ‘kimewakata’ wabunge wake zaidi ya 90 waliokuwa wakitetea nafasi zao ndani ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Baadhi ya wabunge waliokatwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli, walikuwa wameongoza kwenye kura za maoni.
Kati ya wabunge hao, walioangukia pua, wamo mawaziri wawili na naibu mawaziri wawili.
Mawaziri hao ni; Dk. Harrison Mwakyembe wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Angellah Kairuki wa Ofisi ya Waziri Mkuu –Uwekezaji.
Naibu mawaziri ni; Omar Mgumba wa Kilimo na Dk. Mary Mwanjelwa wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kati ya wabunge 93, 88 ni wa majimbo, watatu wa viti maalum na wawili walikuwa viti maalum lakini walijitosa majimboni na kushindwa.
Ukiwaacha wabunge hao 93. Kuna wabunge wawili, Profesa Anna Tibaijuka wa Muleba Kusini na John Kadutu wa Ulyankulu wao walitangaza awali kustaafu kuwania ubunge huku Nimrod Mkono wa Butiama yeye hakujitosa kutokana na hali ya kiafya.

Kwa hali hiyo, ukichukua hao 93 waliokatwa na watatu hawakujitosa kwenye mbio hizo, wanafika 96 ambao sura zao hazitoonekana ndani ya Bunge la 12 labda miongoni mwao wateulewe na Rais katika nafasi zake kumi za wabunge.
Baadhi ya wabunge hao waliofyekwa na majimbo yao pembeni ni;
- Dk. Charles Tizeba – Buchosa
- William Ngeleja – Sengerama
- Balozi Rajab Adad – Muheza
- Omar Mugumba – Morogoro Kusini Mashariki
- Balozi Diodorus Kamala – Nkenge
- Dk. Harrison Mwakyembe – Kyela
- Stephen Masele – Shinyanga Mjini
- Julius Kalanga – Monduli
- Maulid Mtulia – Kinondoni
- Abadallah Mtolea – Temeke
- Lolesia Bukwimba – Busanda
- Juma Nkamia – Chemba
- Chacha Ryoba – Serengeti
- Albert Obama – Buhigwe
- Daniel Nsanzugwanko – Kasulu Mjini
- Mbaraka Bawazir – Kilosa
- Goodluck Mlinga – Ulanga
- Suleiman Ahmed Saddiq -Mvomero
- Dk. Shukuru Kawambwa – Bagamoyo
- Dk. Haji Mponda – Malinyi
- Peter Lijualikali – Kilombero
- Victor Mwambalaswa – Lupa
- Haroon Pirmohamed – Mbarali
- Rafael Gashaza – Ngara
- Profesa Jumanne Maghembe – Mwanga
- Hassan Masala – Nachingwea
- Jitu Soni – Babati Mjini
- Isaay Paulo – Mbulu Mjini
- James Millya – Simanjiro
- Emmanuel Papian – Kiteto
- Omar Badwel – Bahi
- Issa Mangungu – Mbagala
- Augustino Masele – Mbogwe
- Venance Mwamoto – Kilolo
- Godfrey Mgimwa – Kalenga
- Mahmoud Mgimwa – Mufundi Kaskazini
- Edwin Sannda – Kondoa Mjini
- Charles Kitwanga – Misungwi
- Oscar Mukasa – Biharamulo Magharibi
- Dk. Pundenciana Kikwembe – Kavuu
- Richard Mbogo – Nsimbo
- Christopher Chiza – Buyungu
- Peter Serukamba – Kigoma Kaskazini
- Profesa Norman Sigalla – Makete
- Kangi Lugola – Mwibara
- Deogratias Ngalawa – Ludewa
- Hassan Kaunje – Lindi Mjini
- William Dau – Nanyumbu
- Jerome Bwanausu – Lulindi
- Rashid Chuachua – Masasi
- Saul Amon – Rungwe
- Dk. Mary Nangu – Hanang
- Hasna Mwilima – Kigoma Kusini
- George Lubeleje – Mpwapwa
- Joel Mwaka – Chinolwa sasa linaitwa Chamwino
- Janet Mbene – Ileje
- Omary Kigoda – Handeni Mjini
- Mary Chatanda – Korogwe Mjini
- Mboni Mhita – Handeni Vijijini
- Edward Mwalongo – Njombe Mjini
- Joram Hongoli – Lupembe
- Greyson Lwenge – Wanging’ombe
- Dk. Dalaly Kafumu – Igunga
- Mussa Ntimizi – Igalula
- Ezekiel Maige – Msalala
- Andrew Chenge – Bariadi
- Dk. Raphael Chegeni – Busega
- Salum Khamis – Meatu
- Daniel Mtuka – Manyoni Mashariki
- Allan Kiula –Iramba Mashariki
- Justin Monko – Singida Kaskazini
- Sixtus Mapunda – Mbinga Mjini
- Mbaraka Dau – Mafia
- Edwin Ngonyani – Namtumbo
- Saada Mkuya – Welezo
- Martin Msuha – Mbinga Vijijini
- Ignas Malocha – Kwela
- Hamoud Jumaa – Kibaha Vijijini
- Ally Ungando – Kibiti
- Khamis Yahya Machano – Chaani
- Makame Mashaka Foum – Kijini
- Sadifa Juma Khamis – Donge
- Bhagwanji Maganlal Meisuria – Chwaka
- Salum Mwinyi Rehani – Uzini
- Haji Amie Haji – Makunduchi
- Shamsi Vuai Nahodha – Kijitoupele sasa linaitwa Pangawe
- Kanali mstaafu Masoud Ali Khamis – Mfenesini
- Jamal Kassim Ali – Magomeni
- Angella Kairuki – Alikuwa viti maalum, akagombea Same Magharibi
- Halima Bulembo – Viti Maalum
- Dk. Mary Mwanjela – Viti Maalum
- Vick Kimata – alikuwa viti maalum, akagombea Kibamba
- Amina Mollel- Viti Maalum

Jamani haririni taarifa acheni uongo
Zanzibar wamefyekwa wangapi?